Wednesday, August 7, 2019

MRADI WA UMEME WA Peri-Ubrban WAZINDULIWA BAGAMOYO.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akifungua kitambaa katika jiwe la msingi, ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban, jana Agosti 06, 2019 katika wilaya ya Bagamoyo.
 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban, jana Agosti 06, 2019 katika wilaya ya Bagamoyo.
...................................  


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu,amezindua Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban Rural Electrification Program) wilayani Bagamoyo ikiwa ni muendelezo wa uzinduzi wa miradi hiyo nchi nzima.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu waziri huyo wa Nishati amesema lengo la serikali ni kuwasha umeme katika vijiji 10,278 ifikapo mwezi Juni 2020, ambapo mpaka sasa vijiji 7,349 tayari vimeshaunganishwa umeme.


Alisema katika mradi huo wanachi elfu sita wa awali wataunganishiwa umeme katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kata za Magomeni, Kerege, Zinga, Kiromo Mapinga na vitongoji vyake katika Halmashauri ya Bagamoyo.


Aliongeza kwa kusema kuwa, hayo yote yanatekelezwa kutokana na uongozi mzuri wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, kusimamia ukusanyaji wa kodi ili fedha zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo kama hiyo.


Naibu waziri huyo wa Nishati ametumia nafasi hiyo kuwaagiza wakandarasi na wasambazaji na wazalishaji  wa vifaa vinavyotumika kwenye miradi ya umeme kuzalisha vifaa vyenye ubora ili miradi inayojengwa iwe ya kudumu.


Aidha, alisema wakandarasi wanapaswa kutumia vifaa vinavyozalishwa na kampuni za ndani ili kuongeza pato la ndani kutokana na kodi za wenye viwanda hivyo.


Nao wasambazaji wa vifaa hivyo wametakiwa kuacha urasimu na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi yao kulingana na mahitaji ya wakandarasi ili vifaa viwafikie wakandarasi kwa wakati nao waweze kutekeleza miradi ndani ya kipindi cha mikataba yao.


Alitoa onyo kwa yeyote atakaejaribu kumkwamisha mkandarasi, kuwa hatua hiyo ni kukwamisha juhudi za wizara, na ukiikwamisha wizara umemkwamisha Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba utakuwa ni miongoni mwa wanaorudisha maendeleo nyuma na serikali haitokuvumilia.


Awali akizungumza mbele ya Naibu waziri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi, Amos Maganga, amesema mradi huo utagharimu shilingi Bilioni 12 . 8 utakapokamilika.


Nae Mbunge jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, amesema anamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi huo ndani ya jimbo lake.


Aidha, amempongeza waziri wa Nishati Medard Kalemani pamoja na Naibu waziri Subira Mgalu kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusimamia vyema miradi ili itekelezwe ndani ya wakati.

 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akikata utepe kama ishara ya kuzindua Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban, jana Agosti 06, 2019 katika wilaya ya Bagamoyo, Kutoka kulia ni Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Dorisi Mwakatobe, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Dailin Leonard Mgweno, kutoka kushoto ni Meneja wa Tanesco Bagamoyo, Daniel Kyando,

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Wakili, Julius Kalolo Bundala, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Salum Mtelela, na Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo, Mwanaharusi Jarufu.
 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akitoa maelekezo kwa viongozi wa kampuni ya SINOTEC ambayo ndiyo inayotekeleza mradi huo katikati ni Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Mwakilishi Mkuu nchini Kenya, kutoka Kampuni ya SINOTEC, Jin Hua, wa kwanza kushoto ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara, SINOTEC Tanzania, Xiong Yuezhou.
 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi, Amos Maganga, akizungumza katika uzinduzi huo.
 
 Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Madiwani wakisalimia katika uzinduzi huo, kutoka kulia ni Diwani wa kata ya Fukayosi ambae pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa, wa katikati ni Diwani wa kata ya Kiromo, Hassan Usinga (Wembe) na wa kwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Kisutu, Aweso Ramadhani.
 
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, (kulia) na Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo, Mwanaharusi Jarufu.
 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo Bundala, kushoto ni
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,
 
 Kulia ni Kaimu Miurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi, Amos Maganga, na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Dailin Leonard Mgweno

Meza kuu, katikati ni Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, kutoka kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi, Amos Maganga, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Dailin Leonard Mgweno,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Wakili, Julius Kalolo Bundala, kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Dorisi Mwakatobe, Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo, Mwanaharusi Jarufu, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,

ULEGA AMUAGIZA MRATIBU WA SWIOFish KUFIKISHA ELIMU YA UFUGAJI WA MAZAO YA BAHARI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega amemuagiza Mratibu wa ‘Mradi wa usimamizi wa uvuvi kusini Magharibi mwa bahari ya hindi (SWIOFish) Flora Luhanga, kufikisha Elimu ya Ufugaji wa Mazao ya Bahari katika Wilaya zote zilizopo katika ukanda wa Bahari ya hindi,



Ulega ameto Wito huo Agosti 06, 2019, katika viwanja vya Ngongo , Manispaa ya Lindi alipotembelea katika Banda la maonyesho ya Nane nane la halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.


Ulega alisema kama mkakati wa Serikali wa kuifanya Nchi kuwa ya uchumi wa viwanda ni wajibu kwa watendaji wa Serikali kuwa wabunifu katika mambo mbali mbali yatakayowawezesha wananchi kukuza vipato vyao.


Alisema Kutokana na uhitaji Mkubwa wa Mazao yanayotokana na Bahari wananchi wanatakiwa kuanzisha ufugaji wa viumbe vya bahari ili waweze kukidhi mahitaji ya soko yaliyopo hivi sasa.


Ulega aliongeza kuwa Baada ya Serikali kufanikiwa kutokomeza Uvuvi Haramu kwa Zaidi ya asilimia 95% hivyo ni wajibu kwa viongozi kutoa elimu inayohusu mazao hayo ya Bahari ili kuwafanya wanachi kutorudia tena uvuvi huo haramu.


Hata hivyo waziri Ulega aliwahakikishia wananchi ambao watajiingiza katika kilimo hicho kuwa na soko la uhakika kwani Serikali imekuwa ikipokea maombi mengi kutoka Nchi mbali mbali kwa Mazao yanayotokana na Bahari kama vile, Jongoo wa Bahari pamoja na samaki kaa (SAGO).


“kama wananchi wanaoishi maeneo ya Bahari watahamasika kufanya ufugaji huu kwa hakika watakuwa na vipato vizuri, mathalani kwa mahitaji ya soko kwa sasa kaa mmoja anauzwa kati ya Tsh, 12,000 hadi 15,000 kwa kilo ambapo ukiangalia ufugaji wake wala hauhitaji gharama kubwa zaidi ya kuzungusha uzio utakaoweza kuingiza maji na kutoka katika eneo la bahari atakalochagua kufugia”


Nae mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Christopha Ngubiagai alisema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakinufaiki na Miradi mbali mbali inayohusu mazao ya Bahari na imekuwa ikifanikiwa kufanya ulinzi katika udhibiti wa Uvuvi haramu kwa kushirikiana na vikundi vya Usimamizi wa Bahari (BMU) vilivyopo katika Wilaya hiyo.


Hata hivyo Ngubiagai aliongeza kuwa Mradi huo wa Ufugaji wa Mazao ya Bahari utaweza kumaliza kabisa Uvuvi haramu pamoja na wanachi kuvua samaki wachanga kwani wananchi watakuwa na kipato cha kutosha hivyo hawatalazimika tena kuvua samaki hao wachanga ama kwa kutumia uvuvi haramu