Saturday, June 29, 2019

RAIS DK. MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WABUNGE WA SADC NA SPIKA JOB NDUGAI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma ambao wameongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na wageni hao Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Tingatinga na Kinyago Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, alipokutana na na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya picha ya kuchora toka Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, huku akishuhudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Ikulu jijini Dar es salaam  Ijumaa Juni 28, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019 PICHA NA IKULU

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUACHA KUNYWA POMBE.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Kinamama wajawazito na wanaonyonyesha Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi wameshauriwa kuacha kutumia vileo ikiwemo pombe na sigara ili kuepuka madhara ya kiafya ambayo yatamkuta mtoto atakae zaliwa.


Ushauri huo umetolewa na Veronica Mrope Muuguzi mkunga wa Kituo cha Afya cha Mji katika Manispaa hiyo leo alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG.


Mrope alisema Utumiaji wa vileo kwa akinamama wajawazito na wanaonyonyesha unapelekea watoto wanaozaliwa kuwa na utindio wa ubongo (watoto mataila) pamoja na tatizo la upumuaji.


Alisema hali hiyo inatokana na kemikali zilizokuwepo kwenye vileo hivyo, ambavyo vinamfikia moja kwamoja aliye tumboni kutoka kwa mama yake ama kwa njia ya kunyonyesha kutoka katika maziwa ya mama huyo.


Mrope alisema ili kuepuka madhara hayo na madhara mengine yanayoweza kumpata Mtoto aliye tumbuni ni vyema Mama Mjamzito akaacha kutumia aina hiyo ya vileo mpaka pale Mtoto wake atakapoacha kunyonya.


Nao baadhi ya Wahudumu wa Baa na Clab wa manispaa ya Lindi walidai kuwa kutokana na uzoefu wao katika mkoa huo wamama wajawazito kutumia pombe kali ni jambo la kawaida.


Mmoja wawahudumu hao ambae hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa madhara ya pombe wanazokunywa kina Mama hao licha ya kuathiri mtoto kiafya lakini pia kunaweza kupeleke hata kutoka kwa ujauzito ama kujifungua kabla ya muda.


“Dada hawa wamama bora hata wangekuwa wanakunywa na kutoka lakini humu kwenye Bar yanayotoke ni mengi wakishalewa tuu pengine wanagombana na kupigana humu humu hivi ikitokea Mama huyo anapigwa tumboni unafikili kitatokea nini kwa mtoto huyo? Aliuliza muhudumu huyo.


Nae salma Abdull Mkazi wa Mpili pili manispaa ya Lindi Mkoani humo alisema anachukizwa na kitendo cha baadhi ya wanawake wanaonyonyesha kutumia vileo kwani vinaathili hata ukuaji wa mtoto.


Salma alidai kuwa wamama wengi wanaotumia pombe mara nyingi hupoteza hamu ya kula hivyo humfanya mtoto anaezaliwa na kunyonya kuwa dhoofu kwa kuwa amekosa chakula chenye vitamin kutoka kwa mama yake.


Dalini Athumani ni Mama mwenye Mtoto Mmoja na ni mkazi wa kata ya mikumbi katika Manispaa hiyo ya Lindi yeye alisema kuwa alikuwa analazimika kutumia Pombe wakati wa ujauzito wake kwa kuwa alisikia kutoka kwa Mashoga zake kuwa ukinywa Bia wakati wa ujauzito hautakuwa na tatizo la kupungukiwa na Damu.


“Mimi nilipokuwa na ujauzito wa huyu mwanangu nilikuwa nashindwa kunywa vile vidonge vyekundu vya kuongeza damu nilvyokuwa napatiwa Kliniki kwa sababu vilikuwa vinanichefua hivyo nikaona njia raisi ya kuongeza Damu ni kutumia pombe na kweli mpaka najifungua sikuwa na tatizo lolote la damu” Alieleza Dalini.


Watafiti wa mambo ya Afya wanasema kuwa, Pombe ni sumu kwa mtoto.


Tafiti zinaonyesha kuwa mama mjazito anapokunywa pombe inaingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu wa mama kisha hufika kwa mtoto kwa kupitia kondo la nyuma (placenta).


Aidha, mara pombe inapoingia kwenye mzunguko wa damu wa mtoto, huathiri uwezo wa mtoto kupata chakula, virutubisho na oksijeni ya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya kawaida katika ubongo na viungo vingine.


Tafiti hizo za kitaalamu katika mambo ya Afya zinaeleza kuwa hali hiyo inaweza kuathiri ubongo wa mtoto na ukuwaji wa viungo vya mwili kwa ujumla.


Uharibifu huo unaweza kuathiri uwezo wa mtoto kujifunza na kufikiri pindi anapozaliwa hali ambayo itajionesha kwa matendo yake kama mtoto na kama mtu mzima.


Aidha, utafiti umeonesha kwamba uwezo wa mimba kustahimili kiwango cha pombe ni mdogo mno hali ambayop huathiri ufanyikaji wa viungo na ukuwaji wake kwa kiasi kikubwa.


Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ni pamoja na

  • Kutoka/kuharibika kwa mimba
  • Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo
  • Mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa mbavu na kidari (sternum)
  • Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya mgongo uliopinda (kibiongo) na vidole vilivyoundana
  • Mtoto kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (microcephaly)
  • Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya pua
  • Kuzaliwa na matatizo ya taya
  • Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona mbali
  • Matatizo ya moyo kama vile moyo kuwa na tundu
  • Matatizo ya figo
  • Mtoto kuwa na ubongo mdogo na pia matatizo ya akili
  • Mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo sungura (lip palate na cleft palate)
  • Matatizo ya kimaumbile ya masikio na ulemavu kwenye sehemu za uzazi (genital malformations).

  • Aina mojawapo ya kansa ya chembe nyeupe za damu (Acute Myeloid Leukemia). Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida moja la utafiti wa kansa la Marekani lijulikanalo kama Journal of the American Association for Cancer Research.

Aidha, utafiti huo umesema kuwa madhara hayo si ya muda bali ya kudumu ambayo yanaweza kusababisha kifo kwa mtoto, malezi na makuzi ya tabu na hata hisia mbalimbali katika maisha.

Wednesday, June 26, 2019

MAKAMPUNI YA KUPULIZIA DAWA KUPAMBANA NA DENGUE MKOA WA DAR ES SALAAM YATAJWA..

SERIKALI PWANI YABAINI CHANGAMOTO 9 BIMA YA AFYA.

Image may contain: 1 person, standing
Na Omary Mngindo, Miono

SERIKALI imeeleza kuwa, imebaini maeneo tisa yaliyochangia kutofikiwa kwa malengo ya mfuko wa Bima ya afya CHF, iliyolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya tiba, kwa wananchi.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mji Mkuu, Kata ya Miono, Halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoani hapa, huku moja ya changamoto hiyo akiitaja kuwa ni mfumo.


Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma yeye amemhakikishia Mhandisi Ndikilo kwamba, atawafikishia wakuu wenzake maagizo yote yliyotolewa ili kuboresha huduma, huku akiwataka wananchi kuchangamkia bima kwa ajili ya kujipatia huduma ya afya.


Mganga Mkuu mkoani Pwani Dkt. Gunini Kamba ameiambia hadhara hiyo kwamba, faida ya bima ya afya iliyoboreshwa, mojawapo ni mgonjwa kupata huduma ngazi za Kitongoji, Kijiji Wilaya mpaka Mkoa, tofauti na hapo awali.


Awali taarifa ya Halmashauri ya Chalinze ikisomwa na Mganga wa halmashauri hiyo Dkt. Rahimu Hangai, imeeleza kwamba vijiji 83 kati ya 84, tayari vimeshanunua simu, kwa ajili ya kuandikisha wananchi, ambao watanufaika na huduma hiyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA WA USIMAMIZI WA BIMA.

MAGAZETI YA LEO JUNI 26, 2019.