Wednesday, April 3, 2019

RAIS MAGUFULI AAHIDI KUIUNGANISHA KANDA YA KUSINI KIUCHUMI

Rais Dkt John Pombe Magufuli  amewahakikishia wananchi wa Nanyamba, Tandahimba, na Newala Mkoani Mtwara kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya uhakika ili kuunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kujiletea maendeleo yao.


Akizungumza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, Rais Magufuli amesema Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Nanyamba yenye urefu wa kilometa 50 itakayogharimu kiasi cha Tsh.bilioni 86 na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe kutangaza zabuni ya ujenzi wa kilometa zingine na kufikia kilometa 100 na hivyo kuunganisha kwa urahisi nyanda za kiuchumi katika mikoa ya kusini.


“Barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha uchumi mikoa ya kusini, hatuwezi kushindwa kujenga kilometa 100, lengo letu kuu ni kuiunganisha Bandari yetu ya Mtwara na mizigo inayotoa Malawi,” alisema Rais Magufuli.


Aidha Rais Magufuli alisema kuwa katika kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara, ambapo Serikali imetekeleza ununuzi wa korosho kutoka kwa wananchi wenye korosho zaidi ya kilo 1500, na Tsh Bilioni 50 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao, na kwa upande wa wakulima wa korosho wenye kilo chini ya 1500 wamelipwa kiasi cha Tsh Bilioni 578.


Rais Magufuli amewahiza wafanyabiashara walanguzi wa zao la korosho ‘Kagomba’ kuacha kuwadhulumu wakulima wadogo kwa kuwapa bei ambayo hailidhishi huku wakijua wametumia gharama kubwa katika kuendeleza zao hilo, na kusema serikali ya Awamu ya tano haitarudi nyuma kuwatetea wakulima hao.


“Utakuta mtu amelima korosho zake, amenunua madawa, ametumia gharama kuzivuna unakuja kumpa bei ya 1500, kwa Serikali ya Awamu ya Tano hili halikubaliki”, alisema Rais Magufuli.


Akiongelea miradi mingine inayotekelezwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa  ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Mtwara, , upanuzi wa uwanja wa Ndege na ukarabari wa mradi wa maji wa makonde ambao utagharimu kiasi cha Tsh.bilioni 160 zikiwa ni fedha za mikopo kutoka Serikali ya India unaowezesha ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 nchini.

MTENDAJI MKUU TFS AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA MAADILI.

Image may contain: 3 people, people smiling, people standing and indoor
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanznaia Prof. Dos Sanatos Silayo amewataka waajiriwa wapya na wazamani wa TFS watekeleze majukumu yao kadri sheria za nchi na jinsi maadili yanavyowataka.


“ Niwapongeze watumishi wapya kwa kupata nafasi ya kufanya kazi nasi lakini nataka kuwasisitizia kuwa suala la uadilifu na maadili katika utumishi si la mzaha, enendeni mkalitumikie taifa na kamwe msisubiri kufanya kazi kwa kusukumwa!


“Kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa hiari, kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kuhakikisha utumishi wa umma unaleta tija iliyokusudiwa, nanyi watumishi wa zamani tumewaleta katika mafunzo haya ikiwa ni jitiada za kurejesha uadilifu na maadili miongoni mwenu, ” alisema Prof. Silayo.


Kwa upande wake Mkuu wa Mafunzo ya muda mfupi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles Magaya aliyemwakilisha Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo hicho, Dr. Emanuel Shindika aliipongeza TFS kwa kutambua kuwa ili utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia utoaji wa huduma bora, utiii kwa Serikali, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria na matumizi sahihi ya taarifa kwa kuwapa nafasi yakuwafunza watumishi hao.
Image may contain: 2 people, people standing and suitImage may contain: 21 people, people smiling, people sitting

MAENEO 17 DAR KUFUNGWA CCTV CAMERA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiongoza Kikao cha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, kujadili Mradi wa kuweka Kamera za Kudhibiti Uhalifu(CCTV Camera) katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika leo April 03, 2019 jijini Dodoma.

Washiriki wa Kikao cha Wadau wa kujadili Mradi wa Kuweka Kamera za Kudhibiti Uhalifu(CCTV Camera) katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam,Faraji Ntembo na Faizer Mbange(kushoto), wakipitia moja ya nyaraka inayohusu mradi huo wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu. Kikao hicho kimefanyika leo April 03, 2019 jijini Dodoma.
 

Mshiriki wa Kikao cha Wadau wa kujadili Mradi wa Kuweka Kamera za Kudhibiti Uhalifu (CCTV Camera) katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam,Wankyo Nashon akichangia hoja, kushoto  ni mshiriki  Lina Rujweka. Kikao hicho kimefanyika  leo  jijini  Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchia