Tuesday, April 2, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA MKOANI MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia pamoja na Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mtwara wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara hafla iliyofanyika leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakwanza kutoka kulia pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Ujenzi, Wabunge pamoja na viongozi wa mkoa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara.

Kwaya ya chuo cha Utumishi wa Umma Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kushoto pamoja na  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe kulia wakati Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Mtwara na Dar es Salaam ilipoku wa ikitumbuiza uwanjani hapo. PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa upanuzi wa uwanja huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Mtwara mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la mradi wa Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara hafla iliyofanyika leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani humo.

BABA AMNYONGA MWANAE HADI KUFA KIBAHA.

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

JESHI la polisi mkoani Pwani linamshikilia Robison Enerst (33) fundi ujenzi kwa kosa la kumnyonga shingo, hadi kufa mwanae Modesta Robison mwenye umri wa miezi sita, akidai sio mtoto wake.


Kamanda wa polisi mkoani hapo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Wankyo Nyigesa, alieleza kwamba, tukio hilo limetokea april mosi, mwaka huu  huko mtaa wa Vitendo kata ya Misugusugu, Kibaha.


“Kabla ya kuolewa na mtuhumiwa, mama wa mtoto (marehemu)  alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine ambae mtuhumiwa anamtuhumu ndio baba halali wa mtoto “


“Hali hiyo ilisababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wazazi hao “alifafanua Wankyo.


Wankyo alibainisha, wamemkamata mtuhumiwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kabla ya kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.


Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi, kuwa wanapokuwa na mashaka na jambo fulani la kihalifu watoe taarifa mapema katika vituo vya polisi ili yaweze kushughulikiwa mara moja kabla ya kuleta madhara yeyote kwa lengo la kudhibiti watuhumiwa. 


Hata hivyo, baada ya kumhoji mama wa marehemu yeye alidai mtuhumiwa alishafanya majaribio ya kumuua marehemu mwanae mara mbili.


Anaeleza, mara ya kwanza alitaka kumpa sumu ya vidonge lakini mama huyo aliwahi kumuokoa .


“Mara ya pili mtuhumiwa alinoa panga ili amkate mtoto lakini hakufanikiwa pia kufikia april 1, ambapo alimuua mtoto kwa kumnyonga shingo hadi kufariki dunia “

MAGAZETI YA LEO TAREHE 02 APRIL 2019.

Monday, April 1, 2019

WAZIRI WA ELIMU AZINDUA UKUMBI WA KISASA WA MIHADHARA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

Image may contain: 9 people, people smiling, people standing
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako(Katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo Jipya la Kufundishia lililojengwa na chuo hicho kwa gharama za mapato ya Ndani kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephene Wasira
..................................

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezindua ukumbi wa mihadhara wa kisasa katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere uliojengwa mapato ya ndani ya Chuo hicho.


Akizundua ukumbi huo wa Mihadhara kigamboni jijini Dar es salaam Waziri Ndalichako amepongeza Bodi ya Utawala na Uongozi wa Chuo hicho kwa kusimamia vema matumizi ya fedha zinazotokana na Mapato ya ndani na kutumia kutekeleza miradi yenye tija kwa Chuo na Taifa kama ilivyofanyika katika ujenzi wa Ukumbi huo na pia amewataka uongozi kusimamia Dira na Dhima ya uanzishwaji wake kwa kujikita katika kutoa mafunzo ya Uongozi, Utawala na Maadili.


Waziri Ndalichako amewapongeza Watendaji wa Chuo kwa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mradi huo hadi kufikia hatua ya kukamilisha japo kwa kuchelewa kwa karibu miezi tisa.


“ nimefurahishwa na kazi hii nzuri iliyofanyika hapa, kwakweli ni jengo zuri lenye ubora wa hali ya juu na ambalo litawafanya wanafunzi kuongeza ari ya kujifunza na ninategemea kuona jengo hili likituzwa vizuri ili litumike kwa miaka mingi likiwa na ubora uleule”.


Amesisitiza Ndalichako
Aidha Ndalichako amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuthamini na kutumia vizuri mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutekeleza mipango na Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika taasisi hizo ili kuleta maendeleo ya haraka badala ya kuzitumia fedha hizo kwa matumizi mengine yasiyo na tija.


Wakati huo amewataka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ni wakandarasi wa ujenzi wa Ukumbi huo kukamilisha miradi mingine iliyo chini ya Wizara ya Elimu ikiwemo ukarabati wa shule Kongwe mfano Kibaha Sekondari, Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea pamoja na ujenzi wa Hosteli na miundombinu mingine katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila.


Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo hicho Stephen Wasira, amesema Chuo hicho kimejipanga kuhahakisha kinatoa elimu bora na wahitimu walio bora wenye weledi hasa katika eneo la uongozi na utawala ili kuenzi fikra na maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alieanzisha chuo hicho Mwaka 1961 kwa lengo la kuandaa viongozi na watawala.


Awali, Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila akitoa taarifa ya mradi amesema jengo hilo limegharimu zaidi ya Shilingi za Tanzania Bilioni 1.1 na kwamba lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 330 kwa wakati mmoja. Ameongeza kuwa pamoja na ukumbi wa Mihadhara jengo hilo lina ofisi nane za wahadhiri na mifumo ya kisasa ya sauti.


BUNGE KUANZA KESHO APRIL 02,2019.