Monday, January 28, 2019

WAWEKEZAJI KUTOKA AUSTRIA WAVUTIWA NA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NCHINI.

Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Austria wenye makazi yake Nairobi, Kenya. Bw. Kurt Muellauer akifungua Kongamano la Biashara lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA) na Ubalozi wa Austria. 

Kongamano hilo nimwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambao unawakilisha pia nchini Austria na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi. 

Pamoja na mambo mengine kampuni 8 kati 16 zinatarajiwa kufanya ziara jijini Dodoma tarehe 29 Januari kwa lengo la kukutana na Mawaziri wa Kilimo; Nishati; Fedha na Mipango; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kongamano hilo limefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC, Bw. John Mnali, pamoja na wadau wengine wakimsikiliza kwa makini Bw.Muellauer (hayupo pichani). 

 Baadhi ya wawekezaji kutoka Austria nao wakifuatilia kongamano hilo.

 Kaimu Rais wa Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Octavian Mshiu, akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji nchini na kuunga mkono Sera ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya Uchumi wa Viwanda nchini.  
 Afisa wa Uhamasishaji Uwekezaji (TIC), Bi. Diana Ladislaus akizungumzia fursa za uwekezaji nchini wakati wa kongamano hilo.
 Majadiliano yanayoonesha dalili ya kuzaa matunda ya ushirikiano kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Austria

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JIJINI DODOMA.

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kamati ya uongozi cha kujadili ratiba za shughuli za Bunge katika Mkutano wa kumi na nne (14) kilichofanyika leo tarehe 28 Januari, 2019 katika ofisi ya Bunge jijini Dodoma, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kumi na nne (14) wa Bunge la 11 unaotegemewa kuanza kesho tarehe 29 Januari, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza  na wajumbe wa kamati ya uongozi wakati wa kikao cha kujadili ratiba za shughuli za Bunge katika Mkutano wa kumi na nne (14) kilichofanyika leo tarehe 28 Januari, 2019 katika ofisi ya Bunge jijini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kumi na nne (14) wa Bunge la 11 unaotegemewa kuanza kesho tarehe 29 Januari, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.
 Wajumbe kamati ya uongozi wakiwa kwenye kikao cha kujadili ratiba za shughuli za Bunge katika Mkutano wa kumi na nne (14) kilichofanyika leo tarehe 28 Januari, 2019 katika ofisi ya Bunge jijini Dodoma,  ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kumi na nne (14) wa Bunge la 11 unaotegemewa kuanza kesho tarehe 29 Januari, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAJAJI, WAKUU WA WILAYA WAWILI

Friday, January 25, 2019

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2018 HAYA HAPA


NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

CSEE 2018 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES



CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET