Sunday, November 4, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA BAGAMOYO MIAKA 150 YA UINJILISHAJI, AFYA NA ELIMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinal Njue ambaye aliongoza Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini mbalimbali wa Kanisa Katoliki, Maaskofu pamoja na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu mara baada ya Misa iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kardinali Pengo wapili kutoka kushoto waliokaa, Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinali Njue wapili kutoka kulia waliokaa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ndani  na nje ya nchi mara baada ya Misa ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki mara baada ya Misa ya ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa wanawasili kwa maandamano katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya Misa takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa pamoja na Spika Mstaafu Anne Makinda wakiwa katika Misa takatifu ya ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa kabla ya kuanza kwa Misa takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kardinali Pengo wapili kutoka kushoto waliokaa, Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinali Njue wapili kutoka kulia waliokaa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ndani  na nje ya nchi mara baada ya Misa ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

KUHUSU USHOGA TANZANIA, SERIKALI YAHESHIMU MIKATABA YA KIMATAIFA.

WAZIRI KIGWANGWALA AFANYA UTEUZI WAJUMBE WA BODI YA TAWA.

Kufuatia uamuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, wa kumteua Meja Jenerali (Mstaafu) Hamisi R. Semfuko kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania – TAWA, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb.), amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya TAWA kama ifuatavyo:

1.   Dkt. James V. Wakibara
2.   Dkt. Fredy S. Manongi
3.   Bw. Robert C. Mande
4.   Bi Sauda K. Msemo
5.   Luteni Kanali Christian A. Ng’habi
6.   Dkt. Andrew M. Komba
7.   CP Suzan S. Kaganda
8.   Dkt. Fabian M. Madele
9.   Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA (Dkt. Allan J.H. Kijazi)
10.                Mkurugenzi wa Wanyamapori (Kwa mujibu wa Sheria)
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2018.