Wednesday, October 24, 2018

SAMIA SULUHU AZINDUA KIWANDA CHA MABATI BAGAMOYO.

Mkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akizindua kiwanda cha African Dragon kata ya Zinga wilayani Bagamoyo.

Kiwanda hicho kinazalisha malighafi za mabati ya kuezekea.
 
Meneja Mkuu wa kiwanda cha African Dragon ambacho kinatengeneza malighafi za kutengenezea mabati ya kuezekea Mr. Shi Li Xiong akisoma Taarifa ya kiwanda hicho mbele ya Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan.
   
Meneja Mkuu wa kiwanda cha African Dragon, Mr. Shi Li Xiong akikabidhi Taarifa yake kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akibadilishana mawazo na Meneja mkuu wa kiwanda cha African Dragon, Mr. Shi Li Xiong (kulia) anaesikiliza katikati ni Meneja wa mauzo wa kiwanda hicho, Mr. Andrew.

 
Mkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassanakisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa mara alipowasili wilayani Bagamoyo kuanza ziara ya kikazi mkoa wa Pwani.


Viongozi wa CCM wilaya wakiwa kwenye shughuli hiyo
 Wafanayakazi wa kiwanda cha African Dragon


Hizi ndio malighafi zinazozalishwa kiwandani hapo.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi alioambana nao pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha African Dragon kilichopo kata ya Zinga Bagamoyo, kutoka kulia wa kwanza ni Mkuu wa wilaya ya BagamoyoZainabu Kawawa, wa pili ni wa tatu ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha African Dragon na kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, wa pili ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditie na watatu ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo.



UTIAJI SAINI MKATABA WA MGAWANYO WA UZALISHAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA (PSA)

Mkurugenzi mtendaji wa  Kampuni ya Rakgas L.L.C ya Ras Al Khaimah Bw.Kamal Mohamed Ataya(kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Makazi Mhe.Salama Aboud Talib (katikati) Mkurugenzi Katika Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta Zanzibar (ZPDC)Nd,Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed wakitia saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na Gesi asilia(PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi na Rakgas sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Mtawala wa Ras Al Khaimah Shaikh   Saud bin Saqr  Al  Qasimi wakati alipofanya ziara ya kuitembela Zanzibar mara alipofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar  kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na Gesi asilia(PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi na Rakgas

Picha na Ikulu.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 24 OKTOBA 2018.