Monday, October 22, 2018

WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZOTE NCHINI WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANATOKOMEZA MALARIA.

 
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka Halmashauri nchini kupambana na kudhibiti maambukizi  ya malaria ili taifa kuondokana na tatizo hilo na hivyo badala ya kuhangaika – muda na gharama – na matibabu, kutoa nafasi kwa wananchi kuendelea na ujenzi wa taifa wakiwa na afya njema .

Akizungumza katika uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa viashiria vya malaria nchini, wa mwaka 2017, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka watendaji hao wakuu; wakuu wa wilaya na wakuu wa halmashauri zote nchini kupambana na maambukizi ya malaria ili kutokomeza tatizo hilo nchini
“… mwezi Mei, 2015 Kasulu, Kigoma, kwenye maadhimisho ya siku ya malaria duniani tulizindua takwimu za awali ambazo zilionesha kiwango cha malaria kimeshuka toka asilimia 14 hadi asilimia 7 huku mikoa ya Kigoma asilimia 24.4, Geita asilimia ni 17.3, Mkoa wa Kagera asilimia 13.4 na Mtwara asilimia 14.8 … malaria bado ni kubwa, kwa hiyo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika halmashauri hizo, wafanye kazi ya kusimamia kazi ya kutokomeza malaria”, Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy alisema kuwa katika utafiti huo unaonesha kuwa kila Halmashauri zina asilimia kadhaa za kiwango cha malaria, kwa maana viwango hivyo havikatishi tamaa kwa watendaji wa halmashauri kuchukua dhamira madhubuti ya kupambana na maambukizi ya malaria katika maeneo yao ili kutokomeza kabisa tatizo hilo, kama mpango wa Serikali wa kupambana na malaria unavyobainisha.

Aidha, Waziri aliongeza kuwa, katika hali ya kudhibiti kiango cha malaria, Serikali ina mpango wa kushusha kiwango hicho hadi kufika chini ya asilimia moja ifikapo 2020, kadhalika kutokomeza kabisa malaria ifikapo 2030, ili kuwawezesha wananchi kufanya kazi wakiwa na afya njema.
“tumeweka malengo kwamba kufikia 2020 tunataka kiwango cha malaria kifikie chini ya asilimia moja, na ifikapo 2030 tuwe tumetokomeza kabisa malaria nchni.” Amesisitiza Waziri.

Akaongezea kwa mfano, kwa Mkoa wa Kigoma ambapo halmashauri zake kiwango ni kikubwa zaidi, zikwemo Halmashauru za Kakonko (asilimia 30.8), Kasulu (asilimia 27.9), Kibondo (asilimia 25.8),  Uvinza (asilimia 25.4), Kigoma (asilimia 25.1), Buhigwe (asilimia 24) na Kigoma (asilimia 25.1), halmashauri hizi na nyinginezo, Wakurugenzi pamoja na watendaji wengine eneo la afya na jamii, wanapaswa kufanya kazi na wananchi ili kuweza kuondoa tatizo hili.

Kwa upande mwingine, wananchi wametakiwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri kutunza mazingira yao kwa kufukia madimbwi, kujenga vyoo bora, kukata nyasi na kuzoa taka katika maeneo yao,na kwamba itapunguza vifo vinavyosababishwa na malaria, kwani takwimu nchini zaashiria vifo vya watoto ni 33 kati ya watoto 1000, wakati Serikali imelenga, kama si kutokomeza vifo, basi vifikie hadi watoto 9 kati ya watoto 1000.

KAMISHNA MKUU WA TRA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WAKE KUHUSU UBORESHAJI WA HUDUMA MBALIMBALI ZA WALIPAKODI

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza leo na watumishi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi waliopo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam juu ya uboreshaji wa huduma mbalimbali za walipakodi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza leo na watumishi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi waliopo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam juu ya uboreshaji wa huduma mbalimbali za walipakodi.
Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Gabriel Mwangosi (katikati) akitoa maoni wakati wa kikao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Bi. Agnes Kitwanga akifafanua jambo wakati wa kikao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya watumishi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wakimsikiliza kwa makini Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (hayupo pichani) wakati wa kikao na kamishna huyo kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO) KUPITIA FULLSHANGWE BLOG.