Wednesday, October 17, 2018

SERIKALI IMEZITAKA HALMASHAURI KUANZISHA ONE STOP CENTRES KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI NCHINI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Engineer Evalist Ndikilo  kuhusu masuala Afya pamoja na Maendeleo ya Jamii mapema leo ofisini kwake Kibaha Mkoani Pwani.
.........................................
Serikali imezitaka Halmashauri  zote Nchini kuhakikisha zinakuwa na vituo vya huduma za  mkono kwa mkono (Ones Stop Centre) ili kuunga mkono serikali katika juhudi zake za kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.


Hayo yamesema leo wilayani kibaha mkoani Pwani na Naibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea kituo cha huduma za mkono kwa mkono kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa lengo la vituo hivyo linalenga kupunguza mlolongo wa huduma kwa muhanga wa ukatili kwani vituo hivyo vinatoa huduma za matibabu, huduma za polisi na ushahuri wa kisaikolojia kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema nchi kwa sasa ina vituo kumi tu hivyo kutaka maeneo Mikoa mingine kuiga Mkoa wa Pwani kuunga mkono juhudi hizi kwa kuwa takwimu zilizopo zinaonesha Tanzania ina matukio ya ukatili 41,000 na kati ya matukio hayo 13,000 ni ukatili dhidi ya watoto akitaja hali hiyo kuwa ni ujambazi mpya dhidi ya binadamu.

Amezitaja juhudi nyingine za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kuwa ni kuwepo kwa madawati ya Jinsia katika vituo vya polisi akitaja idadi ya vituo hivyo kote Nchini kuwa ni jumla ya madawati 500.

Ameongeza kuwa Serikali inawajengea uwezomwalimu wa Shule za Msingi na Sekondari ili kuwa na madawati ya ukatili wa kijinsia kwani vitendo vingi vya ukatili kwa watoto vinatokea katika eneo la shule.

Dkt. Ndugulile pia ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili vinavyotokea katika maeneo yao hasa nyumbana katika familia na amesema Serikali itawachukulia hatua watoa huduma za fya watakaojihushisha na uitoaji wa taarifa za uongo kuhusu mashauri ya vitendo vya ukatili.

‘’Baadhi ya wanajamii hapa nchini wanafurahia vitendo vya ukatili kwani wamekuwa wakimalizana kifamilia na kusababisha vitendo hivi kuendelea” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Naibu Waziri Ndugulile ameuagiza Mkoa wa Pwani pamoja na mikoa mingine Nchini kuanzisha dawati la ulinzi wa wanawake na watoto akiongeza kuwa ili ni agizo la serikali hivyo ni lazima mikoa yote Nchini inakuwa na madawati haya ili kutekeleza agizo la serikali.

Akiongea na watumishi wa hospitali ya Tumbi Dkt. Ndugulile amesema kumekuwepo  na kasumba ya adaktari ya kuficha ushahidi kwa watu waliofanyiwa vitendo vya ukatili na kuongeza kuwa hilo ni kosa kisheria na atakayebainika kuficha ushaidi adhabu yake ni kufutiwa usajili.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile yupo katika ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Pwani anmbapo anatembelea na kukagua huduma za afya na maendeleo ya jamii.
 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugezi Mkuu wa hospitali ya Tumbi Dkt. Edward Wayi akitoa maelezo ya Kituo cha Mkono kwa Mkono (one stop centre) kwa waandishi wa habali kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia mapema leo Tumbi Kibaha Mkoani Pwani.

NACTE LATAKIWA KUHUISHA MITAALA ILI IENDANE NA SOKO LA AJIRA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na watumishi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE (hawapo pichani) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao.
.....................................


Serikali imelitaka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha Vyuo inavyovisimamia vinahuisha mitaala yake kila baada ya miaka mitatu kwa mujibu wa sheria ili kile kinachofundishwa kiweze kuendana na mahitaji halisi ya soko kwa sasa ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia.


Kauli hiyo ya Serikali imetolewa  na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha jijini Dar Es Salaam alipofanya ziara katika Taasisi hiyo ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kutembelea Taasisi zilizo chini ya Wizara na kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao.

Ole Nasha alisema ufundi ni taaluma ambayo inabadilika kila siku hivyo ni vyema mitaala ikapitiwa ili kozi zinazotolewa ziendana na ushindani wa soko la ajira.

Pia Naibu Waziri Ole Nasha amelitaka Baraza hilo kuendelea kufanya ukaguzi wa vyuo vyake na kuvifutia usajili vyuo vyote ambavyo havifuati sheria, kanuni na taratibu ikiwa ni pamoja na kuvichukulia hatua vinavyoendelea kufanya makosa kwa mujibu wa sheria.

“Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) tangu mwaka 2016 imefungia vyuo 74 ambavyo havifuati taratibu wakati mwaka huu vyuo 3 vimefungiwa huku vingine 21 vikizuiliwa kutoa baadhi ya kozi hii ni kutokana na dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano iliyo nayo ya kuhakikisha Elimu itolewayo ni bora na sio bora Elimu” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.

Katika hatua nyingine ameipongeza NACTE kwa kusimamia vizuri udahili wa wanafunzi kwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifumo 14 ya TEHAMA ambayo imesaidia zoezi la udahili kufanyika kwa ufanisi hatua iliyopelekea kuongeza idadi ya wanafunzi elfu kumi zaidi kutoka ile ya mwaka jana ambayo walidahili wanafunzi 110,000.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ni Serikali ambayo imejipambanua katika kufikia uchumi wa kati na wa Viwanda ambao ili uweze kufanikiwa uanahitaji mafundi waliosoma vizuri, hivyo elimu ya ufundi ni moja ya vipaumbele vya Serikali na kuzitaka Mamlaka hizo kusimamia elimu itolewayo ili tolewe kama inavyostahili.

Naibu Waziri amehitimisha ziara yake ya siku moja jijini Dar es Salaam kwa kutembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi VETA ambapo amewataka kuandaa vijana ambao ni mahiri na wabobezi katika fani mbalimbali watakaofanya kazi katika viwanda ili kujenga uchumi wa viwanda.

Watumishi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha alipofanya ziara katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Makao makuu jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO 17 OKTOBA 2018