Tuesday, January 23, 2018

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEKETEZA ZANA ZA UVUVI HARAMU CHATO



 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega  akiteketeza nyavu haramu  zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 wilayani Chato.
 .............................

Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega leo ameteketeza zana haramu katika Ziwa Victoria zikiwemo Nyavu za Makila zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 pamoja na Pikipiki tano zilizokuwa zikitumia katika kusafirisha Samaki haramu.

Akizungumza na wananchi wa Mwembeni Wilayani Chato Mhe.Ulega amewata kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kuwafichuwa haralifu hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini ama kwenda jela.

”Serikali haitamuonea mtu huruma awe kiongozi au Raia wa kawaida Sheria itachukuwa mkondo wake nia yetu nikuona Samaki wanaongezaka ziwa Victoria na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taifa liweze kupata mapato pamoja na ajira kwa wananchi mbalimbali” amesema Mhe.Ulega 

Aidha Naibu Waziri huyu amewaonya Wafanyakazi wa Hifadhi ya Rubondo kuacha tabia ya kupewa rushwana wavivu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua na kuwapatia fedha laki mbili hadi tatu.

Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa victoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi  haramu pamoja na  mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Aidha kiongozi wa oparesheni bwana Gabriel Mageni aliongeza kuwa  katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na tatu baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na  baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa pamoja na Madiwani wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni  wanaofanya shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha hasara Serikali ikiwemo kukosa mapato
mapato.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Chato  ,Shaban Ntalambe ,amewataadhalisha  watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu kuwa endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo awe kiongozi Mkubwa ama mtu wa kawaida.

Mkuu  wa Wilaya Chato,Shaban Ntalambe akishiriki zowezi la akiteketeza nyavu haramu .
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Mwembeni pamoja na watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akiwa ameambatana na  Mkuu  wa Wilaya chato,Shaban Ntalambe wakielekea katika kisiwa cha hifadhi ya Lubondo.

aibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Lubondo juu ya kuacha kushirikiana na wavuvi haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua.

SUBIRA MGALU ACHANGIA UJENZI WA SHULE KIJIJI CHA KONGO BAGAMOYO.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu, ambae pia ni Naibu Waziri wa Nishati akiangalia Jengo la madarasa mawili katika shule ya msingi Kongo iliyopo kata ya Yombo wilayani Bagamoyo, kulia ni Diwani wa Kata ya Yombo, Mohamed Usinga na katikati ni Diwani wa viti maalum Yombo Elizabeth Shija. 
..................................

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu amechangia bati 30 katika ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Kongo iliyopo kijiji cha Kongo kata ya Yombo wilayani Bagamoyo.

Subira Mgalu ametoa ahadi hiyo ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa alipotembelea katika shule hiyo hivi karibuni.

Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Pwani ambae pia ni Naibu waziri wa Nishati alitembelea shuleni hapo ili kuona kazi ya kufikisha umeme katika shule hiyo inavyoendelea.

Alisema amefurahishwa na juhudi zilizofanywa na wananchi katika kuchangia miradi ya maendeleo hivyo nae anaungana nao kwa kutoa bati 30 kwaajili ya kuezekea madarasa hayo.

Akizungumza na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mbunge huyo ambae ni Naibu waziri wa Nishati alimtaka mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kongo kuboresha taaluma kwa wanafunzi wake ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Alisema kufuatia kuingia umeme katika kijiji hicho ambao utafika katika shule hiyo ni wazi kuwa elimu pia itaboreshwa katika shule hiyo ukilinganisha na awali kabla ya kuwa na umeme.

Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na jukumu lake la ubunge wa mkoa wa Pwani kupitia viti maalum atafuatilia maendeleo ya shule hiyo ili kuona kama kutakuwa na mabadiliko ya ufaulu baada ya shule hiyo kupata umeme.

Awali Mkuu wa shule hiyo Sadiki Abasi  alimueleza  Naibu waziri huyo kuwa kumekuwa na mazingira magumu katika kutayarisha maandalio ya masomo kwa walimu wa shue hiyo hivyo ujio wa umeme utawaongezea ubora katika kufundisha.

Akizungumzia ujenzi wa madarasa mawili yanayojengwa shuleni hapo, Mwalimu mkuu huyo alisema anamshukuru Diwani wa kata ya Yombo Mohamedi Usinga kwa kutafuta wahisani na kuwashirikisha wananchi na hatimae jengo limefkia hatua ya kupauliwa.

Mpango wa ujenzi wa kuongeza vyumba vya madarasa katika shule za wilaya ya Bagamoyo umeasisiwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga kwa kushirikiana na madiwani wa Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze katika kuhakikisha kila shule inaondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa.

Katika mpango huo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo pamoja na madiwani wa kata zote za Bagamoyo na Chalinze  wameweza kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo na kuweza kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa huku wananchi nao wakijitolea katika kazi zilizo ndani ya uwezo wao ili kufanikisha azma hiyo

Shule ya msingi Kongo ina zaidi ya wanafunzi 700 huku ikiwa na upungufu wa vyumba vya madarasa sita ambapo jengo hilo likikamilika kutakuwa na upungufu wa vyumba vinne ili kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa shuleni hapo.
 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu, ambae pia ni Naibu Waziri wa Nishati, akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuhusu ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu, ambae pia ni Naibu Waziri wa Nishati, (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kongo Sadiki Abasi wa kwanza kulia.
 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu, ambae pia ni Naibu Waziri wa Nishati, akiondoka katika shule ya Msingi Kongo, kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa.