Wednesday, January 10, 2018

VIWANDA BAGAMOYO KUINUA PATO LA WANANCHI.



Mkuu wa Wialaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga (wa pili kulia) akipata maelezo ya mtaalamu na msemaji wa Kampuni ya Euro Plastic LTD, Ally Ornek (kulia kwa mkuu wa wilaya, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hokan PindiEuro Plastic LTD
 ........................................

Ujenzi wa viwanda wilayani Bagamoyo unatarajiwa kuinua pato la wananchi na kuingozea mapato serikali kupitia uzalishaji wa bidhaa ndani ya viwanda hivyo.

Katika ziara ya kutembelea viwanda vilivyojengwa  kata ya Zinga wilayani Bagamoyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Alhaj, Majid Mwanga aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kutoa ajira kwa wakazi wa Bagamoyo ili wananchi wakazi wa Bagamoyo wafaidike na uwepo waa vinda hivyo.

Alisema anafahamu katika kutoa ajira kunazingatia sifa za mwombaji ili kukidhi mahitaji ya kazi inayokusudiwa lakini Bagamoyo waapo vijana wasomi na wenye sifa ambao wanaweza kujituma kwa uzalendo wa Bagamoyo yao na nchi yao kwa ujumla.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya aliwatoa wasiwasi wawekezaji kuhusu tatizo la umeme na kusema kuwa Tayari Shirika la umeme nchini TANESCO wilaya ya Bagamoyo limejipanga kuondoa tatizo la umeme ili kuimarisha uzalishaji wa viwanda hivyo.

Katika kuhakikisha  ujenzi wa viwanda unaimarika wilayani Bagamoy, TANESCO chini ya Wizara ya Nishati inatarajia kupeleka umeme mkubwa chini ya mradi wa North East -3 ambao utaweza kutoa jumla ya 220 KV ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu umeme wa wa eneo la Zinga kufikia mpaka 132 KV.

Aidha, TANESCO wanatarajia kuweka Power plant eneo la Zinga yenye uwezo wa kuzalisha takriban Megawatt 200.

Lakini pia TANESCO ili kuhakikisha umeme huu unakuwa wa uhakika wanatarijia kujenga Bomba la gesi kutoka Tegeta hadi Bagamoyo eneo la Viwanda.

Akizungumzia swala la maji alisema tayari DAWASA wanajenga Tanki kubwa la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita milioni sita ambazo zitasambazwa kwa wakazi wa Bagamoyo pamoja na eneo la viwanda.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo amempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia vyema sera ya viwanda kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Akizungumzia fursa za ajira msemaji wa Kampuni ya Euro Plastic LTD, kuoka nchini Uturuki, ALLY Ornek alsema katika viwanda wanavyotarajia kujenga vinaweza kuajiri wafanayakazi zaidi ya elfu tano.

Alli aliongeza kuwa zaidi ya vitano vianatarajiwa kujengwa vikiwemo viwanda vya kutengeneza bomba za Plastic, Vipodozi, na Kiwanda kikubwa cha Nondo.

Miongoni mwa viwanda ambavyo Mkuu wa wilaya aliweza kutembelea kata ya Zinga, ni pamoja na kiwanda cha African Dragon ltd, ambacho kinachakata mabati kabla kuwekwa migongo, kiwanda cha Phiss Turney ambacho ni cha kuchakata ngozi, kiwa cha Eco Consumer Product kinachotengeneza vipodozi pamoja na vifungashio vya bidhaa vikiwemo kopo na chupa za bidhaa mbalimbali.

Aidha, kiwanda kingine ni kile kinachotengeza chakula cha mifugo mbalimbali. 


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa kiwanda cha Euro Plastic LTD pamoja na wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Bagamoyo alipofanya ziara ya kutembelea viwanda vilivyopo kata ya Zinga wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiangaia bidhaa ya mafuta inayozalishwa na kiwanda cha Eco Consumer Product kilichopo Zinga wilayani Bgamoyo, kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Mhandisi Albert Lema.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, akiweka lebo kwenye chupa ya mafuta yanayozalishwa na kiwanda cha Eco Consumer Product wakati alipotembelea kiwandani hapo kujionea shughuli za uzalishaji.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,( wa pili kulia) akiangalia bati ambalo linaandaliwa katika kiwanda cha Arfan Dragon LTD.





TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA ZA MATIBABU



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea kuhusu mikakati ya utendaji kazi kwa mwaka 2018 moja ya mkakati huo ukiwa ni kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa  katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kilichofanyika hivi karibuni. Kulia ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo.

Wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alielezea kazi zilizofanyika katika Taasisi hiyo kwa mwaka 2017  katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kilichofanyika hivi karibuni. Jumla ya wagonjwa  1025  walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kwa mwaka 2017 na hivyo Taasisi kuokoa  zaidi ya bilioni 29 ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nch


Kikao cha kwanza cha Manejimenti  cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka  2018 kikiendelea.

..................................

Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umewaahidi watanzania kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa  kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Ahadi hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kwa mwaka 2018.

Prof. Janabi ambaye  pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho alizitaja ahadi zingine ni pamoja na kuendeea kupunguza kupeleka wagonja nje ya nchi, kupunguza gharama za tiba, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi katika Hospitali na kuendelea  kushirikiana na wananchi.

Mwenyekiti huyo alisema kwa mwaka 2018 wamejipanga  kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ukilinganisha na mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 64,093 walitibiwa katika Taasisi hiyo kati ya hao wagonjwa wa nje walikuwa 60796  na waliolazwa 3297.

“Malengo tuliyokuwa nayo kwa mwaka huu wa 2018 ni kuona wagonjwa wengi zaidi ya hawa tuliowaona mwaka 2017 katika kliniki zetu za kila siku. 

Taasisi imejipanga kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 400 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 1000.Tunatarajia kuwa na kambi maalum za upasuaji wa moyo  zisizozidi 15”.

“Mwezi huu tunatarajia kuwa na kambi mbili zote ni za upasuaji wa bila kufungua kifua. Tunaanza na kambi ya watu wazima  kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani.  Mwisho wa mwezi  tutakuwa na kambi ya watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel”,  alisema.

Kwa upande wa viongozi waliohudhuria mkutano huo Prof. Janabi aliwataka kuwasimamia  wafanyakazi wanaowaongoza ili waweze kufanya kazi  zao kwa ufanisi na uweledi huku wakifuata maadili ya watumishi wa Umma hii itawafanya wananchi waweze kupata huduma bora zaidi.

Nao viongozi waliohudhuria mkutano huo walisema kuwa watahakikisha wanafanya kazi zao kwa kujituma, kufuata kanuni za kazi  na kuwasimamia wafanyakazi wanaowaongoza ili wananchi waweze kunufaika na matibabu ya moyo yanayotolewa katika Taasisi hiyo.

Kwa mwaka 2017 jumla ya wagonjwa  1025  walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua katika Taasisi hiyo ambapo  zaidi ya bilioni 29 (Tshs. 29,725,000,000/=) ziliweza kuokolewa kama wagonjwa hao wangetibiwa  nje ya nchi. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 29.