Wednesday, January 10, 2018

ROLI LA DANGOTE LAKAMATWA KWA KUBEBA MKAA BILA KIBALI BAGAMOYO.



 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, majid mwanga, (kulia) akiwa na askari wa usalama barabarani wakikagua Gari la DANGOTE ambalo limekamatwa kwa kubeba mkaa gunia 78 bila ya kibali ambapo dereva wa gari hilo amekimbia na kuliacha gari kwenye geti laushuru wa mazao ya Misitu Kitongoji cha Sanzale wilayani Bagamoyo.
.......................................

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, majid mwanga kwa kushirikiana na Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS Wilaya ya Bagamoyo amekamata malori yaliyobeba mazao ya misitu ikiwemo Mkaa, na kuni bila ya kuwa na kibali.

Akizungumza na waaandishi wa Habari Mkuu huyo wa wilaya alise magari hayo yaliyokamatwa yanaongozwa na Gari la Mfanyabiashara DANGOTE ambalo limebeba magunia 78 bila ya kibali kwa lengo la kukwepa ushuru na kuisababishia serikali mapato.

Gari hilo la DANGOTE lenye namba za usajili T 751 DKA limekamatwa kufuata doria inayofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS wilaya ya Bagamoyo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa uvunaji mazao ya misitu wilaya ya Bagamoyo ambae ni Mkuu wa wilaya katika kuhakikisha mazao yote ya misitu yanalipiwa ushuru.

Mkuu wa wilaya Majid mwanga alisema kumekuwa na tabia ya magari yanayobeba mizigo aina nyingine kujihusisha na ubebaji wa mkaa kinyume cha sheria huku baadhi ya magari hayo yakiwabandikwa namba za usajili za bandia.

Aidha, Majid aliwaonya wale wote wanaofanya biashara za mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu za kukata lessni za uvunaji na kukwepa kulipa ushuru kuacha mara moja tabia na badala yake wafuate sheria ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kumpata mmilikiwa gari au mwenye mzigo.

Kwa upande wake meneja wa wakala wa huduma za misitu nchini wilaya ya Bagamoyo, Joeli Liyangala alisema kuanzia mwezi wa 11 mwaka jana 2017 hadi januari mwaka huu 2018 jumla ya magunia 1436 ya mkaa yamekamatwa ambayo na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 34 ambapo kati ya hayo Gari lililobebaba magunia mengi zaidi ni gari la GANGOTE.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akikagua magari yanayobeba mazao ya misitu bila ya vibali katika eneo Makurunge
 
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akikagua magari yanayobeba mazao ya misitu bila ya vibali katika eneo Makurunge, wa pili kulia ni meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Joeli Liyangala.


WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA USAFIRISHWAJI WA MBOLEA.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.  kushoto akiongea na Waziri wa Viwanda na  Biashara  (kulia).Bwana Charles Mwijage na  Waziri wa Kilimo (katikati) Dkt. Charles Tizeba pamoja na Maofisa wa JWTZ wakati alipo tembelea Kikosi cha 95KJ kinacho Safirisha Mbolea kwenda Mikoani.
 ....................................

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na usafirishaji wa mbolea kutoka wa wasambazaji wa pembejeo nchini kwenda kwa wakulima.

Pia ameitaka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuwa na mikakati madhubuti itakayowezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati wote nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 10, 2018) wakati akikagua usafirishaji wa mbolea kwenye maghala makubwa matatu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kuona wakulima wote nchini wanapata pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati ili kilimo kiweze kuwaletea tija.

Amesema TFC inatakiwa ianze maandalizi ya usambazaji wa mbolea mapema kwani Serikali inataka wakulima wapate pembejeo miezi miwili kabla ya kuanza kwa msimu.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akutane na wadau na kufanya mapitio ya gharama za usafirishaji wa mbolea.

Amesema lengo la mapitio hayo ni kuhakikisha mkulima aliyeko kijijini anapata  mbolea hiyo kwa gharama nafuu bila ya kumuathiri mfanyabiashara.

Pia amemtakaDkt. Tezeba ashirikiane na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba ili kuhakikisha malori yanayobeba mbolea yanafika katika mikoa husika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo awasiliane na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawala ili malori yanayobeba mbolea yakifika kwenye vituo vya mizani yapewe kipaumbele.

“Si kwamba yaongeze uzito hapana, bali yapewe kipaumbele cha kupima haraka ili yaweze kuwahisha mbolea kwa wakulima kwani tayari msimu umeshaanza.”

Naye Waziri wa Kilimo, Dkt. Tizeba alisema watahakikisha mbolea ya kutosha inakuwepo nchini na kwamba wakulima wote wanaipata kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Maghala aliyoyakagua Waziri Mkuu ni ghala la Mohammed Enterprises lililoko Mbagala, ghala la  Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) lililoko Kurasini na ghala la Premium lililoko Vingunguti ambako kote amekuta malori yakipakia mbolea kwa ajili ya uisafirisha katika mikoa mbalimbali nchini.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 10, 2018.