Friday, January 5, 2018

DC BAGAMOYO AFUNGA MAFUNZO YA MGAMBO.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga, akikagua gwaride kwa wahitimu wa mafunzo ya mgambo (jeshi la akiba) katika viwanja vya shule ya msngi Vigwaza Halmashauri ya chalinze.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga amefunga rasmi mafunzo ya mgambo yaliyoendeshwa ndani ya kata mbili za Makurunge na Vigwaza na kuwataka wawekezaji ndani ya wilaya ya Bagamoyo kuwatumia kwa shughuli  za ulinzi.

Alisema kufuatia viwanda vilivyopo wilayani Bagamoyo wahitimu hao wa jeshi la akiba wanapswa kupewa ajira ili wafaidike na fursa zilizopo ndani ya wilaya yao.

Alisema si vyema kuona wawekezaji wenye viwanda wanachukua walinzi nje ya bagamoyo hali ya kuwa wilaya hiyo imezalisha vijana wenye uwezo, waaminifu na wenye kujituma katka kazi ya ulinzi.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo aliwataka wahitimu hao kuwa waadilifu na kuchunga kiapo cha utii ili watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Akitoa Taarifa ya mafunzo Mshauri wa mgambo wilaya ya Bagamoyo, Kapteni Matonya alisema ofisi yake inatoa shukrani kwa ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kuonyesha ushirikiano kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mafunzo hayo.

Alisema mafunzo hayo yamekabiliwa na chnagamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama za kuchangia michango mbali mbali inayohusu mafunzo kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.

Mafunzo hayo ya jeshi la akiba wilayani Bagamoyo yalianza rasmi Tarehe 01 julai 2017 katika kata za Makurunge na Vigwaza yalikuwa na wanafunzi 176 ambapo waliofanikiwa kuhitimu ni wanafunzi 144 ambao kati yao wanaume ni 121 na wanawake ni 23.

Wahitimu wa jeshi la akiba wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambae ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Ahaj, Majid Mwanga.




Thursday, January 4, 2018

DC BAGAMOYO AZINDUA CHANJO YA VITAMIN "'A'' HALMASHAURI YA CHALINZE


 Mkuu wa  wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga, akimpatia mtoto dawa ya vitamin A ikiwa ni ishara ya kuzindua chanjo ya vitamin A na dawa za minyoo katika kituo cha Afya Chalinze.
Mkuu wa  wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga amezindua chanjo ya vitamin A na dawa za minyoo katika Halmashauri ya Chalinze.

Ktika uzinduzi huo mkuu huyo wa wilaya amewapongeza watumishi wa Afya katika Halmashauri ya Chalinze ambao wanafanya kazi kwa kujituma huku akiwataka kuongeza juhudi katika kuwahudumia wananchi.

Aidha, amewataka wale wenye tabia ya kutoa lugha kali kwa wagonjwa kuacha mara moja na badala yake wazingatie kanuni na taratibu za kazi yao katika kutekeleza majukumu yao ya kitaalamu.

Majid aliongeza kwa kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya vitamin A na na dawa za minyoo ili kuwaepusha na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika.

wakati huohuo aliwataka kinamama kufika mapema katika vituo vya Afya na Zahanati kwaajili ya vipimo ili kubaini endapo kuna tatizo kwa mtoto aliyopo tumboni liweze kushughulikiwa mapema.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mratibu wa Afya Halmashauri ya Chalinze, Dkt. Miriamu Malekela alisema zoezi linaloendelea katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kwamba linatarajia kukamilika Januari 17, 2018

Baadhi ya wazazi waliofika kituo cha Afya Chalinze kuwapatia watoto wao chanjo ya vitamin A na dawa za minyoo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Afya Chalinze.

Sunday, December 31, 2017

KOROSHO ZAINGIZA BILIONI 39 PWANI



Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga.

MKOA wa Pwani ,tayari umeuza tani 19,815 ambazo zimeingiza  zaidi ya bilioni 39 tofauti na msimu uliopita ambapo uliuza tani 13,000 na kupata bilioni 33.##

Mkoa huo umejiwekea lengo la kuuza tani 25,000 hadi 30,000 kwa msimu huu ambao  minada yake ya korosho ikiwa bado inaendelea .

Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyasema hayo Mkuranga ,wakati akizungumzia changamoto na mafanikio waliyoyapata msimu wa korosho 2017/2018 .

Alieleza ,mbali ya hayo wakulima wa korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano.

Mhandisi Ndikilo alisema ,kuuza tani 19,815 hadi sasa ni mwanzo mzuri wa kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu.

Alisema ,hatua hiyo imetokana na serikali kutoa pembejeo bure katika msimu huu na mfumo wa stakabadhi ghalani.

Alibainisha ,licha ya mafanikio hayo lakini kuna changamoto zimejitokeza tangu kuanza kwa minada mwaka huu ikiwemo uhaba wa magunia .

Kero nyingine ni ile iliyojitokeza sasa ya kuchakachua ubora wa korosho unaofanywa na baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika (Amcos).

“Changamoto ya magunia inaweza kuwa historia endapo tutakubaliana kwa kukaa na mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuhamasisha wawekezaji waje wawekeze kiwanda cha magunia lengo likiwa ni kukabiliana na tatizo hili” alifafanua .

Akizungumzia kuhusu tatizo la ubora wa korosho, mhandisi Ndikilo ,alisema baadhi ya Amcos zimejiingiza kwenye kuhujumu minada hiyo kwani baadhi yao wameweka michanga na mawe kwenye magunia ya korosho .

Alisema huo ni wizi,uhujumu uchumi na kuaibisha sifa ya nchi ya Tanzania nje ya nchi kwani magunia hayo yangefika India na nchi nyingine ingekuwa aibu na fedheha.

Kutokana na upuuzi huo ndio maana nimeamua kutoa maagizo kuwa Amcos 10 zilizojihusisha na ubabaishaji huo viongozi wake wakamatwe na kuhojiwa.

Kwa mujibu wa mhandisi Ndikilo ,kuwepo kwa maghala makubwa itainua soko la korosho msimu ujao na kuondoa ubabaishaji wa maghala ya vichochoroni yanayoleta dosari .

Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani  ni mkombozi kwa wakulima hivyo anawashangaa wale wanaobeza na kuyumbisha mfumo huo.

Mhandisi Ndikilo ,aliwataka wakulima wa korosho kuacha kukubali kurubuniwa na madalali ama wanunuzi wachache hali inayosababisha kukosa mapato kulingana na korosho zao.

Serikali mkoani humo imewatoa shaka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa fedha zao na kudai itasimamia makampuni na wanunuzi kulipa kwa wakati na changamoto zinazojitokeza.