Monday, December 11, 2017

IGP ASHRIKI MAZOEZI PAMOJA NA ASKARI WA TABORA


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu toka kulia leo asubuhi alishiriki  mazoezi ya utayari na kuwatia hamasa Askari wa  Mkoa wa Tabora,  katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, hatua hiyo ni kutokana na kuwataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa na utayari wakati wote .
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa amembeba Joshua mtoto wa muumini wa kanisa la Siroham mkoani Tabora kabla ya uzinduzi wa zahanati ya Polisi iliyojengwa kwa hisani ya kanisa hilo. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kushoto akiangalia  mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi akiwa katika mazoezi ya utayari kupita juu ya kamba mkoani Tabora leo.
 Picha na Jeshi la Polisi.

JUKWAA LA WANAWAKE BAGAMOYO LAANDAA MAONYESHO



Jukwaa la wanawake wilaya ya Bagamoyo linaandaa maonyesho kwa wajasiliamali ili kutafuta fursa zilizopo katika jamii.

Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi wilaya ya  Bagamoyo  Teddy Alban Davis amesema wamefikia uamuzi wa kufanya maonyesho hayo baada ya kufanya utafiti wajasiliamali wanawake katika kata 11 za Halmashauri ya Bagamoyo.

Alisema katika vikundi vya wajasiliamali wanawake wilayani Bagamoyo vipo vyenye uezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na zenye kuvutia lakini watambuliki.

Teddy alisema kwa kutumia maonyesho hayo wajasiliamali watapata nafasi ya kuonyesha bidhaa zao na kutambua fursa zilizopo kupitia watu watakaohudhuria katika maonyesho hayo.

Aidha, alisema mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wajasiliamali wa Bagamoyo kujitokeza kwa wingi ili kupata nafasi ya kuonyesha bidha zao.

Mwenyekiti huyo aliwataka wajasiliamali wanawake kuwasiliana na ofisi za kata ili kupata maelekezo ya kushiriki maonyesho hayo.

Alisema maonyesho hayo yatafanyika siku ya tarehe 20-25 Desemba 2017  katika uwanja wa Mwanakalenge ambapo Taasisi mbali mbali zitakuwepo kama TBS, TFDA, SIDO NK.