Sunday, March 5, 2017

IGP ERNEST MANGU ATEMBELEA NCHINI RWANDA KIKAZI.

RW1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Ernest Mangu (Kushoto), akiwasili nchini Rwanda, na kupokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini humo, (IGP) Emmanuel K. Gasana (Kulia) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 RW2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Ernest Mangu, Kushoto akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
RW3
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Ernest Mangu (mbele kushoto) akitoa neno mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, pamoja na ujumbe alioongozana nao nchini humo jana, katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
RW4
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania, (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akimsikiliza mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, akitoaneno mbele ya  wajumbe kutoka Tanzania (hawapo pichani) IGP Mangu, yupo nchini Rwanda, kwa ziara ya siku moja  yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 RW5
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Ernest Mangu (kulia),  na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakibadilishana hati ya makubaliano yenye mkakati wa kuhakikisha nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda, zinakuwa salama hususan maeneo ya mipakani na hata kwenye barabara zote zinazotumiwa na wafanyabiashara, IGP Mangu, pamoja na ujumbe wake amefanya ziara ya kikazi nchini humo jana.
 RW6
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, mara baada ya kuitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda. 
 RW7
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, mara baada ya kuitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.  (Picha zote na Demetrius Njimbwi- Jeshi la Polisi Tanzania)

MEZA YA MAGAZETI LEO 05 MARCH 2017.

MAMA SAMIA MGENI RASMI UKARIBISHO VIONGOZI DODOMA.

Nyerere Square
Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma mahali ambapo kutafanyika sherehe za kuwapokea viongozi mbalimbali wa serikali baada ya kuhamia Dodoma.
..........................

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla maalumu ya kuwakaribisha viongozi wa Serikali itakayofanyika Machi 5 mwaka huu mkoani Dodoma.

Hafla hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma na itafanyika mkoani humo katika viwanja vya Nyerere (Nyerere Square) kuanzia saa 8 kamili mchana.

Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Jeremia Mwakyoma ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya ujio wa viongozi hao katika Mkoa huo.

Mwakyoma amesema viongozi wa Serikali kuhamia katika Makao Makuu ya Nchi ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano hivyo Mkoa utawakaribisha rasmi Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara waliohamia kutoka Jijini Dar es Salaam.

“Tukio la viongozi wa Wizara kuhamia Makao Makuu Dodoma ni la kihistoria ndio maana uongozi wa Serikali ya Mkoa umeona ni vema kuweka utaratibu rasmi wa kuwakaribisha viongozi hao,”alisema Mwakyoma.

Afisa Habari Mwakyoma amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa huo pamoja na Mikoa ya jirani kuhudhuria kwa wingi kwenye hafla hiyo.

Mnamo Julai 25 mwaka 2016 katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yalioadhimishwa mkoani Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli alitangaza rasmi Serikali kuanza mchakato wa kuhamia Dodoma ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Nchi.