Wednesday, November 2, 2016

BARAZA LA MADIWANI ILEJE LIMERIDHIA KUFUKUZWA KAZI WATUMISHI WAWILI KWA WIZI WA FEDHA.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi akiongea wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
.........................................


BARAZA la Madiwani Wilayani Ileje limebariki kufutwa kazi kwa watumishi wawili wa Halmashauri hiyo kutokanana makosa ya wizi wa mamillioni ya fedha za wafadhili za mradi wa UKIMWI wa Water Reed

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ubatizo Songa amesema kuwa, wameamua kuchukua uamuzi huo mara baada ya kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na  kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Ras wa Songwe na kubaini kuwa, Mganga Daraja la pili Josephat Yisuya na Grace Kibona wameweza kuingizia Halamashauri hasara ya zaidi Milioni 84.

“Josephati aliweza kujipatia kiasi cha fedha shilingi milioni 36254200 /-wakati Grace Kibona Mhasibu Daraja la kwanza aliweza kujipatia Kiasi cha shilingi milioni 48742500/-fedha za mradiwa Water Aid zilizofika katika Halmashauri ya wilaya ya Ileje”alisema Songa

Mwenyekiti huyo ameagiza watu hao kurudisha kiasi hicho chote cha Fedha katika Akaunti ya Halmashauri hili ziweze kufanya kazi zingine.
 
Kwa mtumishi mwengine Anna mwakipesile kesi yake bado inaendelea na uchunguzi wakati huo watumishi 2 baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Ras wa mkoa wa Songwe waliachiwa huru na kurudishwa kazini baada ya tume kuridhika na utetezi wao

Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji Bw Haji Mnasi amewavua vyeo wakuu wa shule wawili ambao ni Henry Musomba wa sekondari Ibaba na Emecka Minga wa sekondari Ngulugulu kwa makosa mabalimbali yakiwemo utoro,uzembe ,lugha chafu na matumizi mabaya ralislimali

Aidha Mnasi alisema kuwa ni wakati wa kila mfanyakazi wa serikalini kujitathimni kwa kile alichofanya kwani waliotuhumiwa ni wengi lakini bado uchunguzi unaendelea hivyo hawajaishia hapo kwani kila mmoja atakayebainika kufanya ubadhilifu sheria itafata mkondo wake.

Ametoa onyo kwa watumishi kuacha kujihusiha na mambo yaliyo kinyume na maadili ya utumishi wa kwa kujiingiza katika masuala ya kifisadi serikali aitamfumbiamcaho kwani hu ni wakatii wa kuwahudumia wananchi wa nyonge kwa maslahii ya Taifa

“Mimi sipo tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa watumishi wazembe nitafuatili utendaji wa watumishi wote wa Ileje ili tuweze kuwatumikia wananchi kama inavyopaswa na kuidumisha kauli ya hapa kazi tu iliyotelwa na rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli” alisema Mnasi  

 

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ileje. 

DC. BAGAMOYO ATOA SOMO KWA MADEREVA WA BODABODA MAPINGA, AWACHANGIA LAKI MOJA KWENYE KIKUNDI.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Majid  Mwanga, akikabidhi  shilingi  laki  moja kwa kikundi cha Bodaboda Mapinga, mara baada ya kuzungumza nao.
 ......................................

Mkuu wa wilayaya Bagamoyo ametoa elimu kwa waendesha Bodaboda wa kata ya Mapinga na kuwataka waache kufanya urafiki wa kimapenzi na wanafunzi ili kuwapa nafasi ya kuendelea kimasomo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wanafunziwengi wasichana hutumia usafiri wa bodaboda kufika shuleni ambapo madereva wa bodaboda hutumia nafasi hiyo kuwalaghai kimapenzi hali inayopelekea wanafunzi kukatisha  masomo kwa kupata mimba na vishawishi vingine.

Alisema jamii inahitaji kina mama walioenda shule ili kusimamia vyema  majukumu yao  na kwamba kina mama wanaotarajiwa  ni hawawasichana wa sasa ambao wanakumbana na changamoto za waendesha bodaboda.
Aidha, aliwataka kutoa ushirikiano kuwafichua wale wote wenye tabia hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Mkuu huyo  wa wilaya aliwachangia shilingi laki moja waendesha boda boda hao katika kikundi  chao ikiwa ni ishara ya kutambua  mchango  wao katika jamii katika kazi wanazofanya huku  akiwasihi  kutovunja sheria  za nchi.




Waendesha bodabodaMapinga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mara alipowatembelea na  kuzungumza nao.