Thursday, September 8, 2016

IGP ERNEST MANGU KUKABIDHIWA UENYEKITI WA SARPCCO MKOANI ARUSHA.

Image result for igp mangu
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI.

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu anatarajia kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) katika mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Septemba, 2016 jijini Arusha. 

IGP Mangu atakabidhiwa uenyekiti huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi ya Msumbiji ambapo atadumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa kamati tendaji za SARPCCO amabazo zitakutana Septemba 14 na 15 mwaka huu  ili kuandaa ajenda na mapendekezo  ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa wakuu wa Polisi ambao unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano huo mambo mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu yatajadiliwa ikiwemo uhalifu wa kuvuka mipaka, pamoja na kuweka mikakati na maazimio ya  kufanya Oparesheni za pamoja zinazojumuisha nchi zinazounda shirikisho hilo.

Vilevile, mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio mbalimbali kupitia kamati tendaji za wakurugenzi  wa upelelezi, kamati tendaji ya sheria, kamati tendaji ya mafunzo na kamati tendaji ya mtandao wa Polisi wanawake.

Aidha, suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo litajadiliwa katika mkutano huo.

SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika katika kukabiliana na uhalifu. 

Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Seychelles.

Imetolewa na:-
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

MAGAZETIYA TANZANIA LEO TAREHE 08 SEPTEMBA 2016.

uhu01

Wednesday, September 7, 2016

MO DEWJI FOUNDATION YAZINDUA MPANGO WA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA UDSM.

DSC_0062
Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez akielezea jinsi wanafunzi hao 10 watakavyoweza kufaidika na udhamini wa Mo Dewji Foundation.
......................................................... 


Mo Dewji Foundation kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM Imezindua rasmi mpango wa ufadhili kwa wanafunzi 10 wa elimu ya juu waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wa 2016 (MO Scholar Program) kwa chuo kikuu cha Dar es salaam leo Jumatano Septemba, 7 2016.

Mpango huu wa ufadhili kwa wanafunzi umelenga kuwawezesha wanafunzi wenye sifa tatu, wasio na uwezo wa kujilipia ada ya chuo, wanafunzi ambao wameshiriki vyema katika michezo na uongozi wakiwa shuleni na wanafunzi ambao wamefaulu kwa kiwango cha alama 1 na 2 (division 1 & 2)

Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez amesema kuwa wameanzisha mpango huo kwa lengo la kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa kutoa msaada wao wa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.

“Mpango wetu kwa muda wa miaka mitatu hadi minne ni kusaidia zaidi Tanzania lakini hapo baadae kama tukifanikisha malengo yetu Tanzania tutakwenda mbali zaidi,” ameongeza Barbara.

Aidha Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi ameelezea kuwa chuo kikuu cha Dar es salaam kimelenga kusaidia wanafunzi wote wa kitanzania ambao wanasifa za uhitaji wa ufadhili na ameomba vyombo vya habari visaidie kusambaza ujumbe kwa watanzania ili wanafunzi wafaidike na mpango huo.

“Tumeanza na chuo Kikuu cha Dar es salaam, tutaangalia namna ambavyo mpango na tutaenda na hapo baadae tutatanua mikono yetu kwenda vyuo mbalimbali,” amesema Barbara.

Na kwa mtahiniwa ambaye anakuwa anahitaji kutuma maombi kwa ajili ya kupata ufadhili wa Mo Dewji Foundation kwa ajili masomo ya chuo kikuu anaweza kuingia tovuti ya modewjifoundation.org

 HHBGHGHDSC_0112

Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi akizungumzia mchakato wa kupata wanafunzi 10 ambao watapata udhamini wa Mo Dewji Foundation.