Wednesday, September 7, 2016

MAKAMO WA RAIS ZIARANI MKOANI MTWARA, AKEMEA UVUVI HARAMU.


5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea
mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
 
Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 mam01
Makamu wa Rais  Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi katika mji wa Nangurukuru Wilaya ya Kilwa waliojitokeza kwa wingi wakati akipita kuelekea Mkoani Mtwara kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
mam1
Makamu wa Rais  Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwasalimia  wananchi katika mji wa Nangurukuru Wilaya ya Kilwa waliojitokeza kwa wingi wakati akipita kuelekea Mkoani Mtwara
mam0001
Baadhi ya wananchi aliojitokeza kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu wakati akipita kwenye mji wa Nangurukuru wilayani Kilwa.
.........................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari ili kudhibiti tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.

Makamu wa Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.

Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.

“Bahari yetu ndio mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu  tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”

Kuhusu uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi zote.

Amesema mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa  la kwanza hadi kidato cha nne.

Katika ziara yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua jengo la ofisi  za Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Makamu wa Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki.

WATUMISHI WILAYANI BAGAMOYO,WAMETAKIWA KUACHA VITENDO VYA RUSHWA.

YO
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Erica Yegella akizungumza na wajumbe wa mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata hawapo pichani  katika  ufunguzi wa kikao kazi maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao katika kutatua migogoro ya ardhi kilichofanyika katika shule ya sekondari Lugoba.

....................................
 
NA VICTOR MASANGU.
WATUMISHI wa umma Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  wametkakiwa kuachana na vitendo vya kuwa na tamaa, ya kupokea rusha au kutoa kwa lengo la kuweza kuuza viwanja kiholela bila ya kuzingatia sheria na utaratibu kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha  kuwepo migogoro ya ardhi ya mara kwa mara kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Yegella kikao maalumu cha mafunzo ya kazi kilichoandaliwa  kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuweza kutimiza majukumu  yao ipasavyo wajumbe wa mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata zilizopo  katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Yegella alisema kwamba watendaji wa ngazi zote kwa kushirikiana na wajumbe wa mabaraza wanapaswa kuitambua vizuri sheria ya ardhi ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa  katika kutatua migogoro ambayo imedumu kwa kipindi cha muda mrefu  ikiwa sambamaba na kutenda haki bila ya kuwa na upendeleo wowote ili kuepukana na vurugu ambazo zinapelekea uvunjifu wa amani.

“Jamani nyinyi ni watendaji hivyo ni lazima kuhakikisha mnafanya kazi kwa misingi ambayo inatakiwa kitendo cha kuuza mashamba au vinnja ni kinyume kabisa na sheria, na kingine tuache tama kabisa ya kufanya mambo bila kuangalia madhara yake kwani baadhi ya maeneo migogoro ya ardhi inachangiwa na baaadhi yetu,”alisema Yegella.

Aidha alisema kwamba ana imani baada ya watendaji hao kupatiwa mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kutatua migogoro ya ardhi ambayo wakati mwingine inapelekea kuwepo kwa vurugu kutokana na kugombania viwanja.

 Naye Afisa kutoka tume ya maadili ya viongozi wa umma  kanda ya Mashariki Seleman Shaban amewataka watendaji nawatumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia maadili na taraibu zote  za kazi zao ili kuepukana na suala la kutoa au kupokea rushwa kwani ni kinyume kabisa  na sheria za nchi.

Jerome Njiwa ni Mwenyekiti wa baraza la ardhi katika Wilaya ya Kibaha ambaye alihudhuria katika kikao hicho na hapa anafafanua zaidi kuhusina na migogoro mingi ambayo imekuwa ikijitokeza katika mabaraza ya ardhi ya kata na nyumba kutokana na kutozifahamu sheria vizuri.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya  kata  na nyumba warioshiriki katika mafunzo hayo  akiwemo Mwinyikondo Asia, Mariamu Swala pamoja na Hassan Ally wamesema kwamba walikuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi katika ufanya maamuzi kutokana na kutozijua vizuri sheria za ardhi.

Mafunzo hayo  ya kuwajengea uwezo wamewashirikisha wajumbe mbali mbali kutoka katika mabaraza ya ardhi ya kata  zilizopo  katika Wilaya ya Bagamoyo  Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kupunguza kero na migogoro ya aradhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na kusababisha vurugu kwa wananchi.

MAGAZETI YA KENYA LEO SEPTEMBA 07,2016.

MAGAZETIYA TANZANIA LEO SEPTEMBA 07, 2016.