Mhe. Nchimbi ametoa kauli hiyo Disemba 15, 2025 Mkoani Kagera baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kampasi ya Kagera ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kutokana na mchango huo, Serikali imejizatiti kuleta mageuzi ya elimu katika ngazi zote, ili kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata ujuzi, stadi na maarifa yanayoendana na soko la ajira.
‘’ Rai yangu kwa UDSM, hakikisheni Kampasi hii mpya inakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu; kuwawezesha vijana wetu kuibua mawazo mapya, kufanya ubunifu, na kutumia fursa za soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki’’ Ameseama Mhe. Nchimbi.
Mhe. Nchimbi ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuratibu mradi mkubwa wa HEET kwa kuhakikisha matumizi adili ya fedha na kwa kuzingatia thamani ya fedha. Ameitaka Wizara kushirikiana na wadau kuandaa mapema mahitaji kama vile ithibati, vifaa na rasilimaliwatu, ili kuwezesha shughuli za mafunzo katika Kampasi hiyo kuanza kama ilivyopangwa bila kuchelewa
Pia ameipongeza UDSM, kwa kusimamia mchakato wa ujenzi wa Kampasi hiyo, ameitaka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika matumizi bora ya rasilimali na utoaji wa elimu yenye tija kwa kizazi cha leo na kesho.
" hapa niwatake wasimamizi mkabdarasi na wote wanauhusika kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati uliopangwa hatutavumilia ucheleqaji wowote" anesema Mhe. Nchinbi
Ameishukuru Benki ya Dunia kwa kushikiriana na Serikali kufadhili utekelezaji wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) , ambao umewezesha ujenzi wa Kampasi ya Kagera hukua akiahidi uwekezaji katika kukamilisha jengo la abweni la wanafunzi wa kiume na miundombinu mingine muhimu.







No comments:
Post a Comment