Viongozi wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Wajumbe wao walioshinda katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024. Leo tarehe 29 Novemba 2024 wameapishwa rasmi kushika nyadhifa zao katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
Akifungua kikao cha kuwaapisha Viongozi hao, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bagamoyo Bw Shauri Selenda aliwakaribisha na kuwashukuru kwa kuchaguliwa na kuaminiwa na wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 27 mwezi huu .
"Nichukue nafasi kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba ya Halmashsuri kwa kuteuliwa kuwa viongozi wa Serikali za Mitaa, "Mchakato haukuwa rahisi lakini mmefanikiwa niwapongeze". Alisema Bw Shauri Selenda.
Katika Uchaguzi huo ulifanyika tarehe 27 Novembe, 2024 vyama mbalimbali vya kisiasa vilishiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwenye vitongoji vyote 167 vya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Shaibu Ndemanga aliwaasa wenyeviti hao kushirikiana ili kuwahudumia wananchi kama walivyoapa katika viapo vyao.
No comments:
Post a Comment