SHEKHE JONGO AKEMEA CHUKI ZA UDINI
SHEKHE JONGO AKEMEA CHUKI ZA UDINI Na Allan Kitwe, Tabora WAUMINI wa dini zote nchini wametakiwa kupendana na kushirikiana katika masuala yote ya kijamii na kiuchumi na kujiepusha na chuki kwa kuwa chuki haileti maendeleo bali inachochea ugomvi na mafarakano. Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Taifa Shekhe Hamid Masoud Jongo kwenye Maulid ya Kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W yaliyofanyika jana eneo la Stendi ya Zamani Mjini Tabora. Ameeleza kuwa hakuna dini inayofundisha chuki miongoni mwa waumini wake au kuchukia dini nyingine, hizo ni fikra ovu za watu au mtu binafsi, hivyo akaonya watu wanaohamasisha chuki au ubaguzi kwa kigezo cha dini. Shekhe Jongo ameweka wazi kuwa Mtume Muhammad S.A.W alijali utu wa kila mtu wala hakubagua yeyote kwa misingi ya dini na kuongeza kuwa vitabu vitakatifu vya dini zote vinasisitiza upendo na amani. ‘Ndugu zangu waislamu, tofauti ya imani sio sababu ya kuchukiana, hata Mwenyezi Mungu hapendezwi na tabia za namna hii, uis...