Thursday, October 28, 2021

BENKI KUU YAONYA MATUMIZI MABAYA YA NOTI.

 No description available.

Hivi karibuni kuimeibuka wimbi la vitendo vya matumizi mabaya ya noti katika shughuli mbalimbali  za kijamii hususan kwenye sherehe za harusi ambapo watu wamekuwa na tabia ya kutunza wahusika  wa matukio kwa kuwarushia noti zinazoanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa, kuziviringisha katika maumbo mbalimbali na kutumia kama mapambo, kuweka kwenye mwili wa  mtu ulio loa jasho na matukio yote yanayofanana na hayo.  

Matendo haya yanatweza fedha ya Tanzania ambayo ni moja ya tunu za taifa letu.Vitendo hivyo  vinaendelea kutokea licha ya Benki Kuu ya Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa nyakati  tofauti kuvikemea. 

Hivyo basi, Benki Kuu ya Tanzania inatoa onyo kwa wananchi ambao bado wanakaidi onyo hili  ambalo limetolewa mara kadhaa kuhusu namna sahihi ya kutunza noti za Tanzania zinazokuwa  mikononi mwao kwa kuzitumia kinyume na maadili pamoja na matakwa ya kisheria. 

Kwa taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania itaanza kuchukua hatua dhidi ya wale wote watakaohusika  na vitendo vya matumizi mabaya ya noti za Tanzania kwa njia yoyote ile ikiwamo kuweka pesa  sakafuni au sehemu yoyote ambayo siyo nadhifu. Vitendo hivyo vinachangia kutweza fedha zetu na kusababisha uchakavu hivyo kuiongezea Serikali gharama kubwa za kuchapisha fedha zingine. 

Aidha, Benki Kuu inawashauri washiriki katika matukio yote ambayo yanahusisha matumizi ya fedha  kuandaa vyombo maalum vya kuweka fedha hizo badala ya kufanya vitendo ambavyo havikubaliki. 

Wananchi wote mnahamasishwa kutoa taarifa mara moja kwa Benki Kuu au Vyombo vya Usalama  pale mnapobaini matumizi yasiyo sahihi ya fedha zetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi  ya wahusika. 

Tukitunza fedha zetu tunachangia kuzifanya zitumike kwa muda mrefu na hivyo kuipunguzia  Serikali

 

MAGAZETI YA LEO TAREHE 28 OKTOBA 2021.

 No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

Wednesday, October 27, 2021

KILOSA KUTUMIA BILIONI 4 ZA IMF KUIMARISHA AFYA NA ELIMU

 No description available.

No description available.

Na Mwandishi Wetu

WILAYA ya Kilosa mkoani Morogoro imepata mgao wa Sh bilioni 4.33 kutoka kwenye fedha zilitolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa Serikali ya Tanzania.

Mgao huo wa Sh bilioni 4.33 uliopelekwa Kilosa na Serikali ni kati ya Sh, trilioni 1.3 ambayo imetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kuwa zitatumika kwenye kutekeleza miradi mbalimbali kwenye sekta ya afya, elimu, maji, viwanda na nyingine.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaj Majid Mwanga amesema fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi mipya kupitia mpango wa maendeleo  kwa usatawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19 ambapo wilaya hiyo imepata fedha kwenye sekta ya elimu na afya.

Alhaj Mwanga amesema Sh bilioni 2.94 zitatumika kujenga vyumba 147 vya madarasa ya shule za sekondari na Sh milioni 780 zitajenga vyumba vya madarasa 39 ya vituo shikizi 13.

“Shilingi milioni 420 zitatunua mashine za mionzi katika Hospitali ya Mikumi, Sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya wagonjwa mahututi na Sh milioni 90 zitajenga nyumba za watumishi,” alisema.

Mkuu huyo amesema wamejipanga kusimamia vizuri mchakato mzima wa ujenzi wa miradi hiyo na kutoa angalizo kwa watu ambao wanatarajia kutumia miradi hiyo kwa manufaa binafsi.

Mwanga amewataka watendaji wote kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilayani ambao wanahusika na utekelezaji wa miradi hiyo kujituma ili miradi ikamilike kwa wakati.

“Kwa niaba ya wananchi na viongozi wa Kilosa, napenda kumshukuru Rais Samia na Serikali yake kutupatia kiasi hiki cha fedha ambacho kinaenda kufanya mapinduzi katika sekta husika. Ninapenda kumhakikishia kuwa tupo pamoja na yeye na hatutavumilia mtu yoyote ambaye atajaribu kuenda kinyume na malengo,” alisema.

Alhaj Mwanga amesema iwapo kila mmoja atatimiza malengo yake kwa weledi ni wazi kuwa Kilosa itabadilika na kupata maendeleo kwa haraka.

 

MKUU WA MKOA WA DODOMA AWATAKA TANROADS KUONGEZA WIGO WA UTOAJI ELIMU

 No description available.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akifungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.

............................................

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ameutaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuongeza wigo wa utoaji elimu juu ya Sheria ya Afrika Mashariki ya udhibiti uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018.

 

Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo ya sheria hiyo kwa wadau wa usafirishaji yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), yanayofanyika kwa siku moja mkoani Dodoma katika ukumbi wa Hazina

 

“Toeni elimu ya kutosha kwa wadau wa usafirishaji nchini, tumieni vyombo vya habari kwa kuandaa vipindi maalum vya redio na televisheni ili kuweza kuwafikia wadau wengi zaidi na hivyo kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa barabara hizi zinalindwa ipasavyo”, amesema Mtaka.

 

Ameongeza kuwa changamoto zinazowakumba watendaji wa mizani kutoka kwa wadau wa usafirishaji, zinatokana na baadhi ya wadau hao kukosa uelewa wa kutosha juu ya sheria ya Afrika Mashariki ya udhibiti wa uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018.

 

Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, amesema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa elimu inayotolewa kwa wadau wa usafirishaji kuhusu sheria hiyo iliyoanza kutumika nchini Machi mosi mwaka 2019.

 

Mhandisi Chimagu amesema kuwa awali Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), ilifanya mafunzo hayo nchi nzima mwezi Oktoba mwaka 2020 na kwamba mafunzo hayo ni jukwaa muhimu la wadau wa sekta ya usafirishaji, kufanya majadiliano kuhusu sheria hiyo, kushauri au kutoa maoni yatakayostawisha utekelezwaji wake.

 

Aidha mmoja kati ya wadau wa usafirishaji Juma Mussa, anayeshiriki mafunzo hayo amewaambia waandishi wa habari kuwa uelewa juu ya sheria hiyo utawasaidia kudhibiti uzito wa magari yao na hivyo kuepukana na makosa wanayoyafanya kwa kukosa uelewa, hali itakayopelekea mtandao wa barabara nchini kudumu kwa muda mrefu bila kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.

 

Mafunzo ya Sheria ya Afrika Mashariki ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 yamepangwa kufanyika katika Mikoa 13 ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Morogoro, Dodoma, Njombe, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Kigoma, Geita, Tabora, Mwanza, Arusha na Tanga, ambapo hadi kufikia sasa tayari, wadau wa usafirishaji katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Morogoro tayari wamenufaika na mafunzo hayo.

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

No description available.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Leonard Chimagu akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (hayupo pichani), kufungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.

No description available.No description available.

Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku moja katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.

No description available.

Watoa Mada wa semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Hazina mkoni Dodoma, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

No description available.

Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

Picha na WUU