Sunday, March 31, 2019

TAARIFA MPYA KUTOKA IKULU LEO MACHI 31, 2019.

RC. NDIKILO AWATOA HOFU BAGAMOYO NA KIBAHA.

 Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia wananchi wa maeneo ya Kibaha na Bagamoyo waliokuwa wanahudumiwa na substation ya Mlandizi iliyopata msukosuko jana wa kuungua moto kwenye moja ya transfoma zake kwamba juhudi zinafanyika ndani ya shirika la TANESCO kufunga transforma nyingine ili nishati ya umeme iendelee kupatikana majumbani kwetu na kwenye maeneo ya uwekezaji vikiwemo viwanda. 


Serikali yetu imejipanga vizuri ili kuhakikisha kwamba tatizo hili halitaathiri shughuli zetu za kila siku za kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla. Hatua za muda mfupi tayari zimeshachukuliwa na shirika la TANESCO ili tuendelee kupata huduma ya nishati ya umeme katika maeneo ya Kibaha na Bagamoyo. 


TANESCO itarejesha tranforma hiyo kubwa kama iliyokuwepo hapo awali ili iendelee kuhudumia viwanda vyetu. Naomba tuwe na subira.

IMETOLEWA NA MKUU WA MKOA WA PWANI
MHANDISI EVARIST NDIKILO.
Image may contain: outdoor

 Hali ilivyokuwa katika kituo cha kupozea umeme cha Mlandizi baada ya moja ya tranforma zake kuungua moto mapema jana Machi 30, 2019.
Image may contain: cloud, sky and outdoor 

Muonekano katika kituo cha kupozea umeme cha Mlandizi baada ya moto kuzimwa kufuatia moja ya tranforma zake kuungua moto mapema jana Machi 30, 2019.

Saturday, March 30, 2019

AMIRI JESHI MKUU RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMETUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) 146 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakati wakielekea kwenda kupiga picha za kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoka katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Maafisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU