Monday, August 14, 2023

DC NYANGASA ATOA USHAURI WA MAENDELEO YA KISARAWE KATIKA DCC

 


KISARAWE PWANI


Mkuu wa Wilaya kisarawe Bi Fatma Nyagasa ameongoza watalaamu mbalimbali katika kikao Cha Kamati ya ushauri wa Wilaya (DCC) Leo 14.08.2023 


Akizungumza wakati wa kikao kilichoendeshwa kwa Mfumo wa taalamu wa Halmashauri ya Wilaya kisarawe Kutoa ushauri Wao kwa mkuu wa Wilaya jinsi ya kuifikisha Wilaya katika Maendeleo yanayotakiwa kwa Mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM alisema Imani alonayo ni Kubwa sana kwa jamii hii ya Kisarawe kupata Maendeleo kutokana na ushauri wanaopata kutoka kwao,


*"Hapa kisarawe kuna watalaamu katika fani Nyingi basi tumieni taluma zenu kuwatumikia wananchi ambao mmetumwa kwenu katika kufanya Kazi ikiwemo Elimu,Afya, umeme, Ardhi, Habari nk*"


*"Kupitia taluuma mbalimbali mlizonazo basi zinufaisheni Halmashauri katika kufanya Kazi kwa uzalendo na kujituma kwa weledi alisisitiza Mhe DC Nyangasa*"


Hata Hivyo kwa Upande wake Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya kisarawe Bi Beatrice Dominic alimhakikishia mkuu wa Wilaya kisarawe kuwa watumishi wote waliopo kisarawe wanafanya Kazi kwa umakini na Ufanisi kwa kuzingatia sheria na kanuni na Kuahidi kuleta matunda Mazuri ya Utumishi,


*"Mhe Mkuu wa Wilaya kwa niaba Yao tukuhakikishie kuwa tunaenda kufanya Kazi kwa umakini na Ufanisi Mkubwa kwa maslahi ya watu wa kisarawe na taifa kwa Ujumla kama ambavyo alimalizia Bi Beatrice*"


Aidha kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya kisarawe Mhe Zuberi kizwezwe, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Komred Halfani Sika, Watalaamu na Wawakilishi wa Tasisi ya Tarura,Ruwasa,Tanesco, TFS, Ardhi,TRA, Nk







 


RAIS SAMIA, CCM, RAI YAO KUONA CHUO HIKI KINAENDA KUFUNDISHA MASOMO YANAOENDANA NA MAZINGIRA YA PWANI -QS KIPANGA

 


NA MWANDISHI WETU


Katika kuelekea hatu za mwisho kwa Mandalizi ya kuanza kwa Masomo katika Chuo Cha Ufundi Veta ndagoni Mkoa wa Pwani Wilaya Mafia, 


Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Kipanga ametoa ufafanuzi kuwa chuo hicho kinaenda kuwa mkobozi kwa taifa kutokana kwa Vijana wambao watajiunga Kusoma Veta ndagoni,


*"Rai ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Veta zote nchini ikiwemo hii ya ndagoni ni kuona Wingi wa Vijana wanaenda kupata maarifa yenye faida kwa taifa ikiwemo Kusoma fani zenye masilahi na zinazoendana na wakati huku zikiakisi Mazingira waliopo kwa ufanisi zaidi ikiwemo Kusoma mambo ya Tehama, Mazingira,pamoja na Mambo ya Uvuvi na bahari alisisitiza Mhe Qs Kipanga*"


*"Maudhui ya Chuo hiki ni pamoja na Kutoa Vijana wenye uwezo wa ambao wakitoka hapa hawatasubiri ajira Bali wanajiajiri wenyewe kupitia maarifa waliyoyapata kuendana na uhitaji Wao muda wote wawapo chuoni alisisitiza Mhe Qs Kipanga*"


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mafia Komred Mohamed Faki alifafanua kuwa Wao kama CCM Furaha Yao ni kuona chuo hicho kinaenda kuwa na Fani mbalimbali ambazo zinaenda kumapatia Kijana Uwanda Mpana Sana wa kuchagua Kusoma kulingana na anachokipenda na kinachomfaa,


*"Hiki chuo ni kikubwa kuliko chuo chochote hapa Mafia na kwa Mkoa wa Pwani ni chuo Cha Veta Cha Kwanza kwa ukubwa wa majengo na Fani zinazoenda kufundishwa basi kiendane na ukubwa wake alimalizia Komred Faki*" 


Mkoa wa Pwani una Veta mpaka Sasa katika Wilaya ya Kisarawe, Rufiji,Mafia nk ambazo zinaategemewa kwenda kusomesha Vijana katika Fani mbalimbali ili kuhakikisha Vijana wanatumia 99%ya vipaji na elimu za Ufundi na ubunifu walio nao katika Mazingira na Fani wanazitaka. 






MLIMA KITONGA KUFUNGWA CAMERA.

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama Barabarani ya Mkoa huo, wapo mbioni kuanza utekelezaji wa mpango kabambe wa kuweka camera za kisasa kwenye maeneo korofi kwenye barabara kuu inayounganisha Mkoa huo na Mikoa mingine na kwa kuanzia camera hizo zitafungwa eneo la Majinja Wilayani Mufindi na Mlima Kitonga Wilayani Kilolo ili kupunguza ajali za barabarani.


Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas @salimasas amesema hayo wakati kamati yake ikiongozwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ilipotembelea maeneo kadhaa ambayo ni korofi na yanayoongoza kwa kusababisha ajali nyingi Iringa.


Asas amesema uwekwaji wa camera hizo utasaidia kupunguza ajali barabarani kwasababu zitakuwa zinafanya saa 24 na zikifungwa Polisi katika Ofisi ya RPC, RTO na OCD watakuwa wanaona LIVE kila kinachoendelea Kitonga na kote zilikofungwa, pia amesema Madereva wakijua eneo lina camera watazingatia sheria za usalama barabarani.


Katika ziara hiyo ya siku mbili Kamati hiyo imetembelea Nyang’oro, Mlima Kitonga na eneo la Majinja ambalo lilipewa jina hilo kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Kampuni ya Majinja Express lililogongana na lori la mizigo na kusababisha vifo vya Watu 50 na wengine 23 kujeruhiwa March 11, 2015


 

MAGAZETI YA LEO TAREHE 14 AGOSTI 2023.

 




























MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWAHIMIZA WATANZANIA KUFANYA KAZI KWA BIDII.

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahimiza waumini na Watanzania kwa ujumla kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kilimo, ufugaji, biashara na kutumikia umma kwa uadilifu ili kuchangia katika ujenzi wa Taifa.

 

Makamu wa Rais ametoa wito huo mara baada ya kushiriki Misa Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma, Misa iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 47 ya Parokia hiyo. Amewasihi viongozi wa dini kutokatishwa tamaa na makwazo mbalimbali wanayokutana nayo katika utume wao na kuendelea kuombea jamii na Taifa zima ili Mwenyezi Mungu aendelee kujalia amani na ustawi.

 

Makamu wa Rais amesema hali ya maadili katika Taifa kwa ujumla hairidhishi ikishuhudiwa kuporomoka kwa maadili na kuongezeka kwa vitendo visivyompendeza Mungu. Ametoa wito kwa wazazi, walezi na walimu kusimamia kiadilifu malezi na makuzi ya watoto na vijana kwa manufaa ya Taifa zima.

 

Halikadhalika Makamu wa Rais amewataka vijana na watoto kuwa na heshima na adabu ili kuweza kukua vizuri na kufanikiwa maishani. Amesema heshima hiyo inapaswa kuwa kwa wazazi, nyumba za ibada, serikali pamoja na mamlaka zingine ambazo zimewekwa na Mungu hapa Duniani.

 

Katika ibada hiyo pia kumezinduliwa kanisani hapo sanamu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu pamoja na kufanyika kwa sherehe ya kumbukumbu ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Msimamizi na Mwombezi wa Parokia hiyo.

 

Ibada hiyo imeongezwa na Padre Africanus Kimario akisaidiwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Emmanuel Mutambo na Mapadre wengine na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali.

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

13 Agosti 2023

Dodoma. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Misa Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma, Misa iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 47 ya Parokia hiyo leo tarehe 13 Agosti 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na serikali mara baada ya kushiriki Misa Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma, Misa iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 47 ya Parokia hiyo leo tarehe 13 Agosti 2023.







RAIS DKT. SAMIA AWAKARIBISHA MADAKTARI BINGWA KUTOKA MAREKANI.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Agosti 13, 2023 amewakaribisha Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka nchini Marekani katika hafla ya chakula cha mchana Ikulu Chamwino Dodoma.


Rais Samia amewashukuru madaktari hao kwa moyo wao wa kujitolea kuwasaidia Watanzania kupata huduma za matibabu ya kibingwa.


Madaktari hao bingwa wameweka kambi katika Hospitali ya Serian Lutherani Jijini Arusha ambapo wanatoa matibabu ya kubadilisha nyonga na goti bure kuanzia Agosti 11 mpaka 17, 2023.


Hafla hiyo imehudhuriwa pia Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Viongozi waandamizi wa Wizara Taasisi za Afya, Madaktari pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Afya nchini.