Wednesday, August 10, 2022

RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUWAHUDUMIA WANANCHI

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Mkoani humo tarehe 10 Agosti, 2022.

******************************

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imezuia kukata na kupandisha hadhi maeneo ya utawala kwa sababu yanaongeza gharama kwa Serikali.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba.

Aidha, Rais Samia amesema mwelekeo wa Serikali ni kunyanyua hali ya uchumi wa nchi ili kuinua hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja.  

Rais Samia pia ametoa wito kwa Viongozi nchini kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa na Serikali ili kuwajengea fursa Watanzania kufanya shughuli za maendeleo na kuinua kipato.

Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi wa Kata, Wilaya na Mikoa kuhudumia wananchi na kutatua kero zao kwa kuzingatia utawala bora.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Soko Kuu la Njombe Mjini mkoani Njombe tarehe 10 Agosti, 2022.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi Soko Kuu la Njombe Mjini katika hafla iliyofanyika mkoani Njombe tarehe 10 Agosti, 2022.

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Njombe mara baada ya kuzindua Soko Kuu la Njombe Mjini tarehe 10 Agosti, 2022.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Tanganyika Wattle ltd Jaswant Singh Rai kuhusu utendaji kazi wa kiwanda hicho ikiwemo uzalishaji wa umeme ambao hutumika kiwandani hapo pamoja na kuiuzia Tanesco kwa ajili ya matumizi ya Wananchi tarehe 10 Agosti, 2022.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyabiashara wa matunda na viatu katika Soko Kuu la Njombe mara baada ya kulizindua Soko hilo tarehe 10 Agosti, 2022

Monday, August 1, 2022

DC MTANDA ASITISHA ZABUNIMPYA YA WAKANDARASI WANAOZOA TAKA HADI KUFANYIKA KWA TATHIMINI .

 No description available. 

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo jijini Arusha .

**************************

Julieth  Laizer ,Arusha

Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda amesitisha  zabuni mpya ya wakandarasi wa kuzoa taka ngumu iliyokuwa ianze agosti mosi  mwaka huu  hadi kufanyika kwa tathimini baada ya kuwepo tuhuma kuna waliopewa zabuni hawana sifa.

 

Mtanda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na ambapo alisema kuwa, amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali juu ya wakandarasi hao kusitisha zoezi la ukusanyaji taka kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kujua hatma yao kutokana na kuambiwa mikataba yao imeisha.

 

 “Mimi malalamiko hayo niliyapata na ninachotaka kusema hapa ni kuwa nawaomba wakandarasi wote waliokuwa wanazoa taka waendelee na shughuli zao za uzoaji taka kama kawaida hadi pale watakapofanyiwa tathmini  kila mmoja na kuweza kupewa mikataba mipya ila kwa sasa hivi nawaombeni mndelee na shughuli zenu kama kawaida.”amesema.

 

Mtanda amesema kuwa,kutokana na kuwepo kwa malalamiko mbalimbali ni lazima wakae chini wafanye tathmini ya utendaji kazi wa wakandarasi hao kipindi cha nyuma kama walifanya vizuri na kama kweli wanakidhi vigezo vya kuendelea na mchakato huo wa uzoaji taka kisheria  na sio vinginevyo.

 

“Nitamwandikia Mkurugenzi  wa Jiji barua kutaka zoezi hilo   na barua hizo zisitishwe na ifanyike tathmini ya kina juu mkandarasi gani alifanya kazi nzuri,yupi aliyelipa fedha ya serikali inavyotakiwa,na wapi hawakufanya vizuri  kwa mwaka huo uliopita na yupi bado anadaiwa fedha na serikali na tathmini hiyo itafanywa na kamati ya  pamoja katika idara ya manunuzi ya jiji,idara ya mazingira ya jiji ili haki iweze kutendeka sitaki mambo ya ujanja katika hili “amesema Mtanda.

 

Ameongeza kuwa, kata ambazo zitaondolewa wakandarasi baada ya tathimini ni zile ambazo zimegundulika kutofanya vizuri na hawataweza kuendelea tena hakuna biashara za kueleana katika hilo,watakaoendelea na zoezi hilo ni wale  waliofanya vizuri na wenye magari ya taka ili waendelee kuwekeza ,hivyo manung’uniko yote yakitolewa ndo mikataba mipya itatolewa na watu kuendelea na kazi katika maeneo yao waliyoomba na sio vinginevyo.

 

Aidha ameagiza  maafisa tarafa wote kuleta orodha ya wakandarasi ambao hawajakusanya taka taka katika kipindi hiki  kwa sababu za kutokuwa na uhakika kama watapatia mikataba mipya au lah kwani kwa kufanya hivyo ni kuhujumu juhudi za serikali za usafi wa mji na mazingira.

 

“Unajua kilichofanyika na jiji la Arusha ni kutoa barua la kusudio la kuingia mkataba rasmi ya wazoa taka katika maeneo mbalimbali,na wakiweka kusudio hatua inayofuata ni kusaini mikataba maalumu kwa ajili ya kuendelea na kazi hizo kila mmoja katika eneo aliloomba baada ya kukidhi vigezo Sasa nasitisha zoezi hilo la utoaji mikataba hadi tathmini ifanyike na kila mmoja ajiridhishe.”amesema Mtanda.

 

Aidha Mtanda ametoa  wito kwa wazoa takataka wahakikishe wanaweka  turubali ya kudhibiti taka zisimwagike  na wataoenda  kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria .