Monday, August 5, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MAADHIMISHO YA AWAMU YA NNE YA WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakimsikiliza  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiongea kabla ya kumkaribisha kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya aendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Reli Tanzania TRC) alipotembelea banda la kampuni hiyo akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya  Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumattu Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege nchini (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi lipotembelea banda la kampuni hiyo akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumattu Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya maendeleo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela katika banda la benki hiyo kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kiatu  wakati alipotembelea banda la Kiwanda cha Viatu cha BORA kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya wakati alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda (UNIDO)  kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba na wafanyakazi wengine wa Shirika wakati alipotembelea banda la TTCL kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Agosti 5, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia burudani wakati akitembelea amabanda kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.

NMB LINDI KUKOPESHA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI.

Hadija Omary, Lindi.

Benki ya NMB Mkoani Lindi imesema itaendelea kushirikiana moja kwa moja na Vikundi vya wakulima, Wavuvi na wafugaji wa Mkoa huo kuwapa mikopo ili kuweza kukuza shughuli zao wanazo zifanya.


Ahadi hiyo imetolewa jana na ofisa wa Benki hiyo Merina Msinza alipokuwa anatoa maelezo juu ya shughuli wanazozifanya mbele ya Mgeni wa Zamu wa maonyesho ya Wakulima (Nane Nane), yanayofanyika Ngongo Manispaa ya Lindi, Sebastian Waryoba.


Msinza alisema katika kuunga jitiada za Serikali za kuinua Uchumi wa jamii ya Watanzania, Benki hiyo imeendelea na itaendelea kutoa mikopo kwa wakulima kama pembejea, matrekta pamoja na pesa Taslimu.


Alisema kwa mwaka wa fedha uliopita zaidi ya Tsh. Miloni 30 Zilikopeshwa kwa vikundi Mbali mbali vya Wavuvi wa Mkoa wa Lindi kwa Wilaya za Kilwa,Lindi Mjini,pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Huku akieleza kuwa pia Benki hiyo imejikita katika utoaji wa pembejeo kwa wakulima wa Korosho pamoja na matrecta ambayo wanayakopesha katika vikundi vya wakulima pamoja na vyama vya Ushirika katika Mkoa huo.


Hata hivyo akizungumza katika Banda hilo La (NMB) katika Maonyesho hayo, Mkuu wa Wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryoba Ameushauri uongozi wa Benki hiyo kufanya Mawasiliano ya Ukaribu na Banki ya maendeleo ya kilimo (TADB) kwa ajili ya Dhamana ya Tahadhari kwa Mikopo inayochukuliwa na wakulima.


Alisema kwa kushirikiana na Benki hiyo ya (TADB) katika utowaji wa Mikopo na kuwadhamini wakulima wao inaweza kuwasaidi namna bora ya kurudisha Fedha Zao za Mikopo zilizokopwa na Wakulima pindi Matatizo yanapotokea.