Tuesday, June 25, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA GHALA NA MITAMBO YA GESI YA KAMPUNI YA TAIFA GAS TANZANIA LIMITED KIGAMBONI, VIJIBWENI, JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz alipowasili kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz kuangalia Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo kabla ya kuvizindua huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Hamisi Ramadhani wakisiliza maelezo ya namna mitambo ya kuchakata gesi inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019. PICHA NA IKULU

TANASCO YATENGA BILIONI 400 KUPELEKA UMEME KWENYE MAENEO YALIYOPITIWA NA MIUNDOMBINU,

Image may contain: 3 people, including Subira Mgalu, people sitting and table
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetenga kiasi cha shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kazi ya kusambaza umeme kwenye maeneo takribani 754 yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme lakini hayana umeme.


Hayo yalisemwa jana tarehe 24 Juni, 2019 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati wa Majumuisho ya Semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyohusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na mradi wa Kinyerezi 1 Extension (MW 185).


Semina hiyo ya siku moja ilihudhuriwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt.Hamisi Mwinyimvua, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo, Menejimenti ya Wizara ya Nishati, REA na TANESCO.


“TANESCO imeshajipanga kufanya kazi hiyo na Wizara inaendelea kusimamia kazi hizi za usambazaji umeme ili kuhakikisha kuwa zinafanyika kwa ufanisi na tumeshafanya vikao mara kadhaa na wadau wanaohusika na usambazaji umeme wakiwemo Mameneja wa TANESCO nchi nzima lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme.” Alisema Naibu Waziri.


Aliongeza kuwa, katika mwaka wa Fedha unaoanza mwezi wa Saba mwaka huu, kipaumbele kitakuwa ni usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali nchini kwani kila siku kuna ziada ya umeme ya kiasi cha megawati 250 hadi 300 kwa siku.


Aidha kuhusu usambazaji umeme katika Taasisi za umma kwenye miradi ya umeme vijijini alisema kuwa, Serikali kupitia REA na TANESCO itaweka kipaumbele cha kupeleka umeme kwenye maeneo hayo ili uwepo wa nishati kwenye vijiji hivyo uwe na tija.


Katika Semina hiyo, wajumbe hao walielezwa mafanikio mbalimbali ya usambazaji umeme vijijini ambapo ilielezwa kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, 2019, jumla ya Vijiji 7,217 kati ya Vijiji 12,268 ambayo ni asilimia 58.9 ya Vijiji vyote vimefikiwa na miundombinu ya umeme.


Pia, hadi kufikia mwezi Juni 2020 jumla ya Vijiji 10,278 sawa na asilimia 84 ya Vijiji vyote vitakuwa vimepatiwa umeme.


Kuhusu utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi I Extension (MW 185) ilielezwa kuwa, mradi huo utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na mkandarasi ni kampuni ya Jacobsen Electro ya Norway.


Katika Semina hayo, Wajumbe hao walitoa maoni mbalimbali yatakayoboresha Sekta ya Nishati nchini ambayo Wizara ya Nishati kupitia Taasisi zake iliahidi kuyafanyia kazi


RAIS, DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA TANZANITE.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 


MAGAZETI YA LEO JUNI 25, 2019.