Friday, May 10, 2019

SERIKALI YAAGIZA MAKAMPUNI YA OCP NA ETG KUFIKIA JULAI 2019 KUWA NA MAGHALA YA KUHIFADHIA MBOLEA –MHE MGUMBA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
.................................

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeyaagiza makampuni ya Premium AgrochemOCP na Export Trading Group

(ETG) kuhakikisha kwamba ifikapo Julai, 2019 kampuni hizo ziwe na ghala za kuhifadhia mbolea na mawakala wa kusambaza katika mikoa inayotumia mbolea kwa

wingi ukiwemo mkoa wa Katavi ili kuondoa changamoto ya upungufu wa mbolea kwa wakulima katika maeneo hayo.


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe Taska Restituta Mbogo aliyetaka kufahamu kuwa serikali ina mpango gani wa kusambaza mbolea kwa wakati katika mkoa wa Katavi.


Alisema kuwa Serikali inatumia Mfumo wa

Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement

System – BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA), Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu

na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.


Mhe Mgumba aliongerza kuwa Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS. 


Alisema Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019. 


Vile vile, ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa
na tani 147,913 za mbolea.


Aidha, Serikali inatumia Mfumo wa Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement System – BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia

(UREA). Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.


Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS. 


Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini

mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019.


Kadhalika, Mhe Mgumba alisema kuwa ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa na tani 147,913 za mbolea.


Serikali imelielekeza Shirika la Reli Tanzania kutoa kipaumbele cha kusafirisha mbolea ili kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja na gharama nafuu ili kumfikia mkulima kwa wakati na bei nafuu” 


Alikaririwa Mhe Mgumba na kuongeza kuwa
Serikali inakusanya mahitaji ya mbegu bora na viuatilifu kutoka katika mikoa ili kuhamashisha kampuni na wafanya biashara kupeleka pembejeo hizo kwa wakulima kabla ya msimu wa kilimo kuanza na wakati wa mauzo ya mazao.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifatilia kipindi cha maswali na majibu wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 10 Mei 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Naibu waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu (Mb) wakifatilia mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 10 Mei 2019.

DC. BAGAMOYO ATOA WITO KUJIUNGA NA CHF.

Image may contain: 5 people, people sitting and indoor
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa ametoa rai kwa Wananchi wa Bagamoyo, hususani Wazee, kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa, ili iwasaidie kumudu huduma za matibabu pale wanapozihitaji.


  Kawaw, ameyasema hayo, hivi karibuni alipokuwa katika hafla maalum ya uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 2000 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.


“Wazee wangu mliofika hapa leo na Wananchi wote wa Bagamoyo, ni vema wote tukumbuke kwamba maradhi huwa hayabishi hodi, na huja bila taarifa, litakuwa jambo la kheri yatakapotufikia tuwe tumejipanga vizuri kwa kuhakikisha kila mmoja wetu amejiunga na mfuko wa Afya ya jamii kupitia mpango wa CHF iliyoboreshwa ambapo itakugharimu kiasi cha Shilingi 30,000/= tu, Mwaka mzima" Alisema.


"Kadi hii ya CHF iliyoboreshwa itakuwezesha kupata huduma bora za afya bure wewe na wategemezi wako 6, katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, Zahanati, Hospitali ya Wilaya na Hospitali kuu ya Mkoa” Aliongeza Kawawa.


Nae mratibu wa dawati la Wazee, kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Rajabu Mturuya katika taarifa yake aliyosoma mbele ya mgeni rasmi amesema, katika kipindi cha Januari – Machi 2019 Idara ya Afya kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii iliwapiga picha Wazee 2000 katika kata za Dunda, Magomeni, Nianjema, Kisutu, Kiromo, Zinga, Makurunge, Yombo na Fukayosi.


Aliongeza kuwa, katika kipindi cha Oktoba – Desemba 2018 kata za Kerege na Mapinga jumla ya Wazee waliopigwa picha ni 349 ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuandaa vitambulisho vya matibabu ya wazee.


Alisema hadi kufikia sasa Halmashauri ya Wilaya kupitia Idara ya Afya, imetoa jumla ya vitambulisho 750 kwa Wazee ambavyo wameanza kuvitumia kwa ajili ya kupata matibabu katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ndani ya Wilaya, hadi kufikia mwezi Juni 2019 Halmashauri inatarajia kutoa vitambulisho 2,000 kwa Wazee wote waliopigwa picha.


Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa amezindua bodi mpya ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambayo imeanza kazi tangu tarehe 13.03.2019 na inatarajiwa kutekeleza majukumu yake kwa muda wa miaka mitatu hadi tar. 13.03.2022.


Mkuu huyo wa wilaya ameitaka bodi hiyo mpya kuhakikisha inasimamia vyema uboreshaji wa utoaji wa huduma za Afya, ili Wananchi wanufaike na uboreshaji wa utoaji wa huduma za Afya uliofanywa na Uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Chini ya Mhe. Rais, Dkt. John Joseph Magufuli, iliyoleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya kwa kujenga vituo vipya vya Afya, Hospitali za Wilaya na utoaji wa dawa na vifaa tiba katika Halmashauri zote Nchini.

 
“Nendeni mkasimamie utoaji wa huduma bora za Afya, Hakikisheni Wazee na Wananchi wote kwa ujumla, wakifika katika vituo vya kutolea huduma wanapokelewa vizuri, hawasumbuliwi na wanapatiwa huduma stahiki kwani Sekta ya Afya ni Sekta yenye changamoto nyingi sana katika masuala ya utoaji huduma na muwe na ushirikiano ili sote kwa pamoja tuhakikishe huduma a Afya kwa Wananchi wa Bagamoyo zinaboreka.


Bodi mpya ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inaundwa na wajumbe 6 ambapo inaongozwa na Mwenyekiti Bi. Roswita F. Kasikila ambaye amemuahidi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo na Wananchi wote wa Bagamoyo kuwa itafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo, kusimamia na kuhakikisha huduma za Afya ndani ya  Halmashauri zinatolewa kwa ufanisi na weledi.


“Tutasimamia uanzishwaji wa dirisha la kuhudumia Wazee, tutashirikiana na Mkurugenzi, kupitia uongozi wa Idara ya Afya kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za Afya kinaanzisha dawati la kuhudumia Wazee, ili Wazee wasiendelee kupata usumbufu wanaoupata sasa wanapofika katika Vituo vya Afya kupata huduma” Alisema Bi. Roswita Kasikila.


Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ina wajibu wa Kuhakikisha jamii inapata huduma bora za Afya inazozimudu, na zinazoimarisha Afya zao, kujadili na kurekebisha mipango ya Afya na bajeti kisha kuwasilisha kwa Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa, kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji kutoka kwa Timu za uendeshaji wa Huduma za Afya Halmashauri, kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato na kukusanya rasilimali za kutosha kuendesha huduma za Afya za Halmasahuri na kusaidia timu za uendeshaji wa huduma za Afya.