Monday, April 1, 2019

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI WAWILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Adolf Ndunguru akiwa pamoja na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wakila Kiapo cha Uadilifu  Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza salamu mbalimbali zilizokuwa zikitolewa Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumuapisha Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) pamoja na Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi wa John Kijazi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji wakwanza kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Adolf Ndunguru  wapili kutoka kulia Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo wapili kutoka kushoto mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


WATANZANIA WATAKIWA KUPANDA MITI KULINDA MAZINGIRA.

Image may contain: one or more people
Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupanda na kutunza miti, ili kujiondoa kwenye athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti.


Mbwambo ambaye aliongoza wadau mbalimbali kupanda miti katika eneo la Kilongawima Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amesema mabadiliko ya sasa ya hali ya hewa ni matokeo ya uharibifu wa mazingira.


Amesema, “Hata mvua zinavyokuwa bila mpangilio ni matokeo ya uharibifu huo, tumeona ipo haja ya kurekebisha hilo na tunafanya kwa kupanda miti,”
“Mwaka huu tumeona tusifanye sherehe za kitaifa kinachofanyika ni kuadhimishwa kikanda kila maeneo watu wanapanda miti na hapa tulipo ni eneo la TFS linalosimamiwa na Kanda ya Mashariki,”


Amesema kwa mwaka huu TFS imeamua kupanda miti katika maeneo ambayo yameathiriwa zaidi na lengo la zoezi hilo ni kuyarudishia kwenye uoto wake wa asili.
Katika eneo la Kilongawima ambalo ni ukanda wa pwani jumla ya miti 1000 imepandwa ikiwemo mivinje na mikoko.


Kwa upande wake Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kinondoni Dotto Ndumbikwa alitoa wito kwa jamii inayozunguka kushirikiana na TFS kuitunza na kuilinda miti hiyo iliyopandwa, na kuahidi kuimarisha doria ya pamoja, na kuwachukulia hatua wale wote watakaofanya uharibifu wa miti kwa kuingiza mifugo kama vile ng'ombe na mbuzi.
Image may contain: 2 people, outdoor and natureImage may contain: 1 person, smiling, standing, outdoor and nature