Monday, April 1, 2019

SERIKALI YAKABIDHI NDEGE YAKE YA FOKKER 50 KWA ATCL

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akipeana mikono na marubani wa ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli  kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Nyuma yake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho,Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Injinia Emmanuel Korosso.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho baada ya kukagua ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikal kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida  kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli  kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Nyuma yao Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka.

Ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikali  kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli   katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akipeana mikono na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho baada ya kumkabidhi ndege serikali aina ya Fokker 50 ili aikabidhi kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida  kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu,Dkt. Moses Kusiluka na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Injinia Emmanuel Korosso.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho baada ya kukagua ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikal kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida  kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli  kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Nyuma yao Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt.Moses Kusiluka.

Wafanyakazi wa ATCL wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Ndegeaina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikali  kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019

MAGAZETI YA LEO TAREHE 01 APRILI 2019.

Dkt Kikwete: Watoto wenye usonji wanastahili kupendwa, kuthaminiwa kama wengine msiwafiche ndani










Na Selemani Magali
Rais  mstafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewataka jamii, walezi na wadau kuwapenda, kuwajali na kuwathamini watoto wenye ugonjwa wa usonji, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwapa furaha.

Dkt Kikwete amesema watoto wenye matatizo ya usonji (Autism) wapo sawa na watoto wengine kinahitajika ni malezi yenye upendo kutoka kwa jamii ili nao wajihisi wako sawa na watoto wengine hapa Nchini.

Dkt Kikwete ametoakauli hiyo mapema hii leo wakati akizungumza katika viwanja vya shule ya AL-MUNTAZIR baada ya matembezi kwa ajili ya kueneza uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ugonjwa wa usonji kwani nao ni watu kama wengine ambao wanaweza pewa fursa ya  kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

Watoto wenye hali ya usonji wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye ugonjwa huu wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.

“Mfano wa hali hii ni kwamba katika hali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi.

 Wadau wanasema Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa walimu na wenzao.