Thursday, January 5, 2017

KINANA NA UJUMBE WAKE WAENDA ZANZIBAR LEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi waandamizi wa CCM katika boti wakati wakiwa safarin kwenda Zanzibar kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la  Dmani, mkoa wa mjini Magharibi, leo. 

Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstafu Lubinza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif khatib.
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi waandamizi wa CCM katika boti ya  wakati wakiwa safarin kwenda Zanzibar kwenye uznduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la  Dmani, mkoa wa mjini Magharibi, leo. 

Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstafu Lubinza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif khatib.
 
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Msami akiwa na Msimamizi Mkuu wa Blog ya taifa ya CCM, Ndugu Nkoromo, katika boti wakati wakienda Zanzibar na Viongozi hao

SERIKALI YAWEKA MPANGO WA UTAMBUZI NA URASIMISHAJI UJUZI.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikianana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini, (VETA) wanaendesha mpango wa Kutathmini na Kurasimisha Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo.

Katika mpango huu una fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi wako, kupewa mafunzo kuziba mapungufu, kisha kutunukiwa cheti.

Fani zitakazohusika ni: UASHI, USEREMALA, UFUNDI MAGARI-MAKENIKA, UPISHI, UHUDUMU WA HOTELI, BAR NA MIGAHAWA.

Ikiwa unakidhi masharti yaliyotajwa, fika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mji au Wilaya iliyoko karibu uchukue na kujaza fomu za maombi bila malipo. Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 05 hadi 25 Januari, 2017.

Watakaokidhi sifa, vigezo na masharti watajulishwa kwa ajili ya usaili kuanzia tarehe 10 Februari 2017.

Mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na Serikali. Kwa taarifa na ufafanuzi zaidi, wasiliana na Mratibu wa Programu (VETA) hii kwa namba 0715 55 55 85.

IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU

4/01/2017

HALMASHAURI YA CHALINZE YASHIRIKIANA NA MBUNGE KUWALIPA POSHO WENYEVITI WA VIJIJI/VITONGOJI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Wilayani Bagamoyo, Saidi Zikatimu, kulia akizungumza na waandishi wa Habari, Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Edesi Lukoe.

Halmashauri ya Chalinze, Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, imetenga kiasi cha sh.mil 36 katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri hiyo.

Kati ya fedha hiyo wenyeviti hao wanalipwa kila mmoja sh.30,000 kwa mwezi hadi mwezi july mwaka huu itakapokoma bajeti hiyo.

Akizungumzia kuhusiana na mpango huo,kwa waandishi wa habari mjini hapo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu ,alisema halmashauri hiyo imeamua kuwalipa posho wenyeviti hao kwani wanafanyakazi kubwa ndani ya miaka mitano bila kuambulia chochote.

Alisema wameshirikiana na mbunge wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete,kuona namna ya kuwatupia jicho wenyeviti hao wa vijiji na vitongoji.

Aidha Zikatimu alieleza kwamba ,fedha hizo zitawawezesha wenyeviti hao kujikimu na kuondokana na hali ya kuuza ardhi za vijiji kwa visingizio vya kukosa posho ama mishahara.

Alibainisha ,fedha hiyo pia itaweza kuwasaidia wenyeviti hao kuwa na morali na ari ya kuchapakazi kwenye maeneo yao  na wamejipanga kila mwaka watakuwa wakitenga fedha hizo.

“Kiasi hiki cha sh.mil.36 ni fedha watakazolipwa hadi july 2017 na bajeti inayofuata tutaangalia kama kuna uwezekanao wa kuongeza kiasi kilichopangwa katika bajeti hii ama ibakie kiasi kilichotengwa kwenye bajeti hii”alifafanua Zikatimu.

Hata hivyo Zikatimu alisema ,wanachotarajia ni wenyeviti hao kuendelea kuwa wasimamizi wazuri katika vyanzo vya mapato na kuachana na tabia ya kuuza maeneo ya vijiji kinyume na taratibu.

Alisema wanawahamasisha kusimamia vyanzo vya mapato ili kuinua makusanyo hasa ya vyanzo vya ndani ikiwemo vizuizi mbalimbali vya pembezoni na ndani ya mji huo.
 
Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa halmashauri nyingine nchini kuwaangalia wenyeviti hao kwani kwa Chalinze imeshaleta tija ndani ya miezi sita tangu kuanza kwa mpango huo.

Aliiomba serikali na halmashauri hizo ziangalie namna ya kuwatengea fedha wenyeviti wa vijiji na vitongoji kama ilivyo kwa madiwani na wabunge wanavyotengewa posho wakimaliza muda wao,ili waweze kuwa na moyo wa kufanya kazi pasipo kukosa  chochote.

“Halmashauri ni sehemu ya kwanza na serikali kuu ni sehemu ya pili,hivyo halmashauri zionyeshe nia ili serikali ilione hili,kwa kuwapa kipaombele ya kuwatengea fedha bila kuwaacha”.

Zikatimu alisema wenyeviti hao wanasimamia chaguzi mbalimbali na ilani ya CCM hivyo waangaliwe katika suala hilo ili waweze kujiona ni viongozi wanaoaminika kwenye maeneo yao.

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani  Kikwete akizungumza katika moja ya vikao vya  madiwani Halmashauri ya Chalinze.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wakiwa katika moja ya vikao vya Baraza  la madiwani Chalinze.

Monday, January 2, 2017

RAIS MAGUFULI ASEMA UMEME HAUTAPANDA.


magufuli18888888888888888
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amewahakikishia Watanzania kuwa licha ya Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) kuridhia ombi la TANESCO la kupandisha bei ya umeme kuanzia Januari mosi,2017 bei ya umeme haitapanda.

Rais Dkt. Magufuli amezungumza hayo leo Jumapili ya Januari Mosi, 2016 wakati wa Ibada katika Kanisa  la Bikira Maria Mama Mwenye Huruma,Kanisa Kuu Jimbo Katoliki la Bukoba anapoanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.

Rais Magufuli ameshangazwa na kitendo cha watendaji waliopandisha bei ya umeme bila hata ya kushauriana na yeye, Makamu wa Rais,Waziri Mkuu au Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo na hivyo kumshukuru Waziri Muhongo kwa kutengua maamuzi hayo.

”Ninamshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini kwa maamuzi ya kusitisha hayo kwa hiyo umeme hakuna kupanda bei,haiwezekani unapanga mikakati ya kujenga viwanda na hasa katika mikakati mikubwa ya nchi ya kusambaza umeme mpaka vijijini,na umeme huu unaenda kwa watu masikini walioumbwa kwa mfano wa Mungu halafu mtu pekee kwa sababu ya cheo chake anapandisha bei,hili haliwezekani” Alisema Rais Dkt. Magufuli.”

Aidha, Rais Dkt Magufuli ameendelea kuwataka watanzania katika mwaka huu mpya 2017 kuendelea kufanya kazi kwa bidii kama maandiko matakatifu yanavyoelekeza kuwa asiyefanya kazi na asile badala ya kulalamika kuwa fedha zimepotea.

Kwa upande wake,Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba,Askofu Methodius Kilaini,akitoa mahubiri kwa waumini waliohudhuria ibada hiyo amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa uongozi wake imara,huku akisema kupungua kwa urasimu katika ofisi za umma kunatokana na  utendaji kuongezeka na kuwataka wana Kagera na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii na uaminifu.

Mara baada ya Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba,Askofu Desderius Rwoma,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliwatakia heri ya mwaka mpya waumini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.

01 Januari, 2017