Tuesday, August 9, 2016

WANAHABARI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO YA AFRIKA.

bal3

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye  akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la  Afrika na China.
................................................................


Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye amewataka waandishi wa habari  kuwa wazalendo kwa kuandika habari za maendeleo ya  bara la Afrika.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wa   ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum na kueleza kuwa uhusiano baina ya Afrika na China ni wa muda mrefu na umejikita katika kuboresha teknolojia ya mawasiliano na hivyo kukuza uchumi wake.

Aidha aliongeza kuwa ili bara la  Afrika liweze kuelezea historia  yake kwa mataifa mingine  katika kujiletea maendeleo  kuna haja ya kuvijengea uwezo vyombo vya habari katika kutoa habari nzuri zenye manufaa kwa jamii husika.

“Katika karne hii tuliyopo sasa kuna mabadiliko mengi ya  teknolojia  hivyo ni budi kuendelea  kuimarisha ushirikiano ulipo baina ya China na Afrika  ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii zetu kupitia vyombo vya habari  huku tukitunza na kueneza tamaduni zetu” alisema Mhe.Nape.

Waziri Nape alizidi kufafanua kuwa vyombo vya habari katika nchi za bara la Afrika vina  uwezo mkubwa wa kukuza na kueneza  utamaduni, kuhudumia  jamii,kujenga umoja wa kitaifa na  kulinda maslahi ya jamii duniani.

Naye Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing amesema kuwa anafurahishwa na  uhusiano  uonaozidi kuimarika baina ya nchi za Afrika na China na kuahidi kuboresha mawasiliano na mahusiano ili kufikia mafanikio makubwa yaliyokusudiwa.

Mkutano  wa China-Afrika Public Diplomacy Forum umejikita katika kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mahusiano baina ya mtu na mtu na Vyombo vya habari,afya,na tiba asilia.
 bal4

Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadali masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la  Afrika na China.
 bal5
Mshauri wa mambo ya Mawasiliano kutoka Tume ya Umoja wa Afrika Bibi. Doreen Apollos akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
 bal6

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na  Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) wakati  wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
 bal7

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kulia) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(wa pili kulia) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
 bal8
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(kulia) wakionyesha hundi ya shilingi milioni arobaini na tano  zilizotolewa na watu wa China kwa ajili ya kuchangia madawati katika shule za msingi za Dar es Salaam.




HASSAN ABBAS ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO, NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI.

mkur2

Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akieleza mikakati yake ikiwemo kuongeza mbinu za Mawasiliano kati ya serikali na wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
..............................................................................


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza  Bw.Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  na Msemaji Mkuu wa Serikali  kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 kifungu Namba 6(1)(b) kufuatia uhamisho wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene uliofanyika  tarehe 7 Machi 2016 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 Mhe.Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa Wanahabari na Wananchi  kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bw Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.

“Ninawaomba Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mumtambue Bw Abbas na mtoe ushirikiano unaostahili katika utendaji wa kazi zake”.Alisema Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri Nape alimpongeza Bibi Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo kwa  kujituma na kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu na uadilifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo mpya amekubali uteuzi huo na ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu mkubwa na ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo na Watanzania kwa ujumla.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Hassan Abbas  alikuwa ni Meneja Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais inayosimamia Utekelezaji wa Program ya Matokeo Makubwa sasa (President`s Delivery Bureau).
 mkur1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimtangaza Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.