Wanafunzi
wa shule za Bagamoyo wakiwa kwenye maandamano kuadhimisha wiki ya Elimu.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa
Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli, akiongea kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
.....................................
Wazazi
na walezi wilayani Bagamoyo wametakiwa kutoa ushirikiano ili kuwafichua wale
wote wanaowapa mimba wanafunzi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga katika hutuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa
Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli wakati wa maadhimisho ya
wiki ya Elimu.
Alisema
watoto wengi hukatisha masomo kwasababu ya kupewa mimba lakini juhudi za
kukomesha vitendo hivyo zinakwama kutokana na wazazi au walezi kutotoa ushirikiano
kwa vyombo vya sheria ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Aliongeza
kwa kusema kuwa serikali imetunga sheria kali katika kuhakikisha vitendo vya
kuwapa mimba wananfunzi vinakomeshwa ili watoto wa kike wapate elimu ambayo ni
haki yao ya
kikatiba.
Akizungumzia
swala la elimu Amuli alisema kufuatia viwanda vinavyoendelea kujengwa wilayani
Bagamoyo watoto wanapaswa kupewa elimu itakayowanufaisha katika soko la ajira
na ile ya kujiajiri.
Aidha,
alisema serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu inatoa elimu bure kwa wote na
kutoa fedha zitakazosadia upatikanaji wa elimu bure ili kila mtoto apate elimu.
Aliongeza
kuwa walimu wakuu wanapaswa kusimamia vizuri fedha za elimu bure ikiwa ni
pamoja na kuzipeleka kwenye matumizi stahiki ili lengo la serikali liweze
kutimia.
Alisema
kufuatia hali hiyo wazazi na walezi jukumu lao ni kuwapeleka watoto shule na
kuwasimamia ipasavyo.
Awali
akisoma Taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Afisa Elimu Msingi
Peter Fussi alisema kufuatia utoaji wa elimu bure idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa shule za awali na msingi
imeongezeka kutoka wanafunzi 25228 mwaka 2017 na kufikia 27508 mwaka 2018.
Hata
hivyo fussi alisema Halmashauri ya Bagamoyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo mahitaji katika idara ya elimu ya msingi ni vyumba 621
na kwamba vilivyopo ni 292 na hivyo kufanya upungufu wa vyumba vya madarasa ni
329.
Aliongeza
kuwa idara ya elimu sekondari mahitaji ni vyumba vya madarasa 162 yaliyopo ni
madarasa 124 ambapo pungufu ni madarasa 38.
Wiki
ya elimu huadhimishwa kila mwaka ikiwa na lengo la kutoa fursa kwa shule,
serikali na wadau mbalimbali kutathmini changamoto zilizopo na kuzitafutia
ufumbuzi.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ni Uwajibikaji wa
pamoja kwa elimu bora kwa watu wote.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa
Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli akipokea maandamano ya wanafunzi yalipowasili uwanjani.
Wanafunzi wa Chuo cha Wakala wa
Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)wakiongoza maandamano katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika uwanja wa majengo Bagamoyo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli
akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama
anavyoonekana pichani akiwa katika banda la shule ya msingi Nianjema ambapo
alijionea Teknolojia ya habari na namna ya masomo mengine yanavyofundishwa.
Alphoncee
Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM)
ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli
akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama
anavyoonekana pichani ambapo
alijionea namna ya masomo yanavyofundishwa.
Alphonce
Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM)
ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli
akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama
anavyoonekana pichani ambapo akiwa katika banda la ADEM ambapo alijionea namna ya masomo yanavyofundishwa.
Alphonce Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Majid Mwanga
Sehemu
ya wananfunzi walioshiriki maadhimisho hayo ya wiki ya elimu.
Wanafunzi
wa shule ya Mwanamakuka wakionyesha umahiri wao katika maonyesho ya sarakasi