Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango
akihutubia wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa kujadili matumizi ya
takwimu za umaskini na namna bora ya kupima hali ya umaskini Afrika jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Dk.Albina Chuwa akitoa hutuba yake.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Kanda ya Afrika
Mashariki, Roland Van De Geer, akitsoma hutuba yake.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird
akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Repoa, Dk.Blandina
Kilama, akizungumza kwenye mkutano huo.
............................................
MATUMIZI
ya Takwimu rasmi katika kupanga maendeleo ya wananchi kwa nchi
zinazoendelea yamekuwa hayaendi kwa kasi inayotakiwa kimataifa imefahamika.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa
Dar es Salaam leo wakati akisoma hutuba yake katika ufunguzi wa mkutano wa
kimataifa wa kujadili matumizi ya takwimu za umaskini na namna bora ya kupima
hali ya umaskini Afrika.
Alisema
wakati dunia ikiendelea na utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo ya
dunia ya mwaka 2030 yapatayo 17, shabaha 169 na viashiria 231 ni dhahiri kuwa
matumizi ya takwimu rasmi katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake kila
nchi haina budi kuyafanyia kazi ipasavyo.
“Kutokana
na hali hiyo ndiyo maana Benki ya Dunia ikishirikiana na Wizara ya Fedha na
Mipango, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeona umuhimu wa kuwa na mkutano huu wa
kimataifa wa kukutanisha watakwimu, wachumi na fani nyingine za kitaalam
kujadili kwa kina matumizi ya takwimu za hali ya umaskini na tafsiri yake kwa
ujumla na nini kifanyike ili kuboresha zaidi tafsiri ya umaskini” alisema Dk.
Chuwa.
Katika
hatua nyingine Dk.Chuwa alitoa angalizo kwa kuwaomba wadau wote wa ndani na nje
ya nchi kuwa takwimu za hali ya umaskini pamoja na utafiti wa mapato na
matumizi ya Kaya nchini zinatolewa na serikali hivyo zisitumike vibaya
kuichafua nchi kuhusu hali ya umaskini.
Alisema
iwapo itatokea kuwepo kwa matumizi mabaya sheria ya takwimu ya mwaka 2015
pamoja na kanuni zake tayari zimesainiwa zitachukua mkondo wake.
Alisema
Takwimu zitumike kwa lengo la kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi maskini wa
Tanzania na kwa nchi zinazoendelea hususan kwa nchi zilizoko Kusini mwa Bara la
Afrika.
Mgeni
rasmi wa mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Benki ya Dunia, Waziri
wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango alisema ilikuweza kujenga Afrika lenye
neema nilazima kuhakikisha kuwa bara hili linaondokana na umaskini na kuwataka
wataalamu waliohudhuria mkutano huo kutunganjia bora ya kupima umaskini.
Alisema
ili kuendana na kasi ya dunia na utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo
ya mwaka 2030 yapatayo 17 ni wazi ufanyaji takwimu na utafiti unapaswa
kufanyika ili kujua kiwango cha umaskini lakini pia aina ya umaskini
uliopo.
No comments:
Post a Comment