Monday, October 10, 2016

MAMA JANETH MAGUFULI AHUDHURIA MSIBA WA SHEMEJI YAKE RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE BAGAMOYO

sal2
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa leo katika makaburi ya mwanakalenge Bagamoyo mjini leo Tarehe 10 Oktoba 2016.sal1
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Saburi,  shemeji yake Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa leo  katika makaburi ya mwanakalenge Bagamoyo mjini leo Tarehe 10 Oktoba 2016.sal3

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa katika makaburi ya mwanakalenge Bagamoyo mjini leo Tarehe 10 Oktoba 2016.
 sal4

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mkwewe Bi Maguno Binti Athumani kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam saburi  aliyefariki jana na kuzikwa leo katika makaburi ya mwanakalenge Bagamoyo mjini leo Tarehe 10 Oktoba 2016.
 sal5

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa katika makaburi ya mwanakalenge Bagamoyo mjini leo Tarehe 10 Oktoba 2016.
 sal6

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwafariji watoto wa Marehemu Mariam Saburi ambaye ni  Shemeji wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa katika makaburi ya mwanakalenge Bagamoyo mjini leo Tarehe 10 Oktoba 2016. 
PICHA ZOTE NA IKULU


WAZIRI UMMY MWALIMU ASEMA DAWA MUHIMU KUPATIKANA MASAA 24 MSD.

Image result for ummy mwalimu images
DAWA muhimu za binadamu zinapatikana kwa wingi katika Bohari kuu ya dawa MSD kwa masaa 24 zikiwemo dawa za kutibu Malaria, Kifua kikuu, Ukoma ,ARV , dawa za kutuliza maumivu pamoja na Anti- biotic ili kutimiza na kutekeleza sera ya mpango wa Afya wa awamu ya tano.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ili kuzungumzia hali ya upatikanaji wa dawa na chanjo nchini.

“Dawa zote muhimu kwa binadamu zinapatikana kwenye bohari kuu ya dawa kwa masaa 24 kinyume  na watu na Taasisi zisizo za kiserikali kusambaza maneno kuwa MSD imeishiwa dawa kitendo ambacho sio cha kweli dawa zipo na zinasambazwa kwenye vituo vyote vya afya” Alisema Mhe. Ummy.

Aidha Ummy amesema kuwa ili kutekeleza mpango wa sera ya afya ya Serikali ya tano ,jumla ya shilingi bilioni 251 zimetengwa ili kuweza kuhakikisha dawa za binadamu zinapatikana kila wakati pindi zinapohitajika kutoka MSD ili kutoa huduma bora kwa watanzania.

Aliongeza kuwa Serikali imetenga Bilioni 85 kwa ajili ya kulipa deni linalodaiwa na MSD ili kuhakikisha Bohari hiyo inajiendesha vizuri na kutokaukiwa dawa pindi zinapohitajika katika vituo vya afya na kutoa huduma za matibabu kwa muda muafaka kwa watanzania.

Mbali na hayo Waziri huyo amesema kuwa tatizo la chanjo kwa sasa limepata ufumbuzi kwani zimeagizwa chanjo za watoto za kifua kikuu dozi milioni 2,  chanjo za Pepopunda dozi  milioni 1.2 na chanjo za Polio ambazo ni dozi 2 ili kuimarisha hali ya matibabu nchini.

“Tulikuwa na tatizo la chanjo kama wiki nne zilizopita lakini tumejitahidi na tumeweza kuleta chanjo zote muhimu pamoja na kuagiza chanjo za surua ambazo zinatarajiwa kuja hivi karibuni ili kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa wingi nchini” alisisitiza Waziri huyo.

Aidha amesisitiza kuwa wanahitaji kununua na kufanya uzalishaji wa dawa katika viwanda vya ndani ili kuweza kuchangia uchumi wa viwanda vya ndani ili tufikie uchumi wa kati.

Waziri Ummy aliwataka Wakurugenzi wa Vituo vya Afya pamoja na Waratibu wa Afya wa Wilaya kuagiza dawa MSD mapema  bila ya kusubiri ziishe kabisa kwenye vituo vyao ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.