Thursday, December 18, 2025

HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA KWA WALIMU WAKUU.

 


Halmashauri ya mji wa Bagamoyo, imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa walimu wakuu wa shule za kata za Zinga, Dunda na Kata ya Yombo.



Makabidhiano hayo yameongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo Mhe Mohamedi Usinga  Desemba 17,2025.


Katika makabidhiano hayo Mhe Mwenyekiti amekabidhi jumla ya komputa (Desktop)44 katika Shule ya Msingi Yombo wamepata Komputa 20,shule ya Msingi Kizuiani 12 na Shule ya Zinga 12 pamoja na Komputa Mpakato moja kwa kila shule na vifaa vyake kwa ujumla.


Mhe Usinga ametoa wito kwa walimu hao kuhakikisha wanavitunza na kuvilinda vifaaa hivyo kwa ajili ya kujifunzia kwa wanafunzi mashuleni ili kuendana na kasi ya teknologia.


Vilevile Mhe Mwenyekiti ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anawezesha upatikanaji wa vifaa vya Tehama mashuleni lakini pia na kuwezesha miundombinu bora mashuleni.


Nae Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo Ndg Shauri Selenda amewasisitiza walimu hao kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo Pamoja na kuhakikisha wanatoa elimu iliyobora kwa wanafunzi ili kujenga msingi bora wa elimu katika Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo.


Aidha Ndg Selenda ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuhakikisha kila shule inakuwa na miundombinu bora lakini pia inapata vifaa vya kujifunzia mashuleni.


Kadhalika Afisa Elimu awali na Msingi Bi Wema Kajigili akitoa shukrani kwa niaba ya Walimu hao wote amesema kuwa “naendelea kutoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassani Pamoja na wadau wote wa elimu nchini vifaa hivi tutahakikisha tunavitunza na kuvilinda na kuhakikisha mwanafunzi ananufaika na vifaa hivi kwa kuwapatia elimu bora”.Bi  Wema Kajigili.







Monday, December 15, 2025

RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 9 WA CDF NA MAKAMANDA.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekufungua mkutano wa 9 wa CDF na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga leo tarehe 15 Desemba 2025. 







π—¦π—˜π—žπ—§π—” 𝗬𝗔 π—˜π—Ÿπ—œπ— π—¨ π—œπ—‘π—” π— π—–π—›π—”π—‘π—šπ—’ π— π—žπ—¨π—•π—ͺ𝗔 π—žπ—”π—§π—œπ—žπ—” π—¨π—–π—›π—¨π— π—œ π—ͺ𝗔 π—§π—”π—œπ—™π—” - π— π—›π—˜. π—‘π—–π—›π—œπ— π—•π—œ


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa sekta ya Elimu, hususan elimu ya Juu ina mchango mkubwa  katika uchumi wa Taifa, kutokana na kuzalisha nguvukazi inayoshiriki kutoa huduma katika sekta mbalimbali.  

Mhe. Nchimbi ametoa kauli hiyo Disemba 15, 2025 Mkoani Kagera baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kampasi ya Kagera ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kutokana na mchango huo, Serikali imejizatiti kuleta mageuzi ya elimu katika ngazi zote, ili kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata ujuzi, stadi na maarifa yanayoendana na soko la ajira. 


‘’ Rai yangu kwa UDSM, hakikisheni Kampasi hii mpya inakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu; kuwawezesha vijana wetu kuibua mawazo mapya, kufanya ubunifu, na kutumia fursa za soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki’’ Ameseama Mhe. Nchimbi.


Mhe. Nchimbi ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuratibu mradi mkubwa wa HEET kwa kuhakikisha matumizi adili ya  fedha na kwa kuzingatia thamani ya fedha. Ameitaka Wizara kushirikiana na wadau kuandaa mapema mahitaji kama vile ithibati, vifaa na rasilimaliwatu, ili kuwezesha shughuli za mafunzo katika Kampasi hiyo kuanza kama ilivyopangwa bila kuchelewa 


Pia ameipongeza UDSM, kwa kusimamia mchakato wa ujenzi wa Kampasi hiyo, ameitaka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika matumizi bora ya rasilimali na utoaji wa elimu yenye tija kwa kizazi cha leo na kesho. 


" hapa niwatake wasimamizi mkabdarasi na wote wanauhusika kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati uliopangwa hatutavumilia ucheleqaji wowote" anesema Mhe. Nchinbi

 

Ameishukuru Benki ya Dunia kwa kushikiriana na Serikali kufadhili utekelezaji wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) , ambao umewezesha ujenzi wa Kampasi ya Kagera hukua akiahidi uwekezaji katika kukamilisha jengo la abweni la wanafunzi wa kiume na miundombinu mingine muhimu.









DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UTATU WA ASASI YA SIASA, UKINZI NA USALAMA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ Troika) uliofanyika kwa njia ya mtandao akiwa Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 15 Desemba 2025.

 


Mkutano huo umejadiili hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kurejesha amani na usalama katika Jamhuri ya Madagascar.




Mkutano huo pia umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe.

UN Secretary-General: Tanzania is a ‘Reference Point for Peace’, Calls for Meaningful National Dialogue Post-Election

 


"Tanzania continues to stand as a reference point for peace and social cohesion in Africa and the world."


These were the words of the United Nations Secretary-General, H.E. AntΓ³nio Guterres, today upon receiving a Special Envoy carrying a message from the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan.


The message was delivered by the Special Envoy, H.E. Ambassador Mahmoud Kombo, the Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation, who led the Tanzanian delegation to the United Nations Headquarters in New York.


Secretary-General Guterres noted that Tanzania’s reputation as an icon of peace was tested during the General Elections held on 29 October 2025, and acknowledged the country’s resilience in maintaining national unity and stability.


He expressed the United Nations’ strong interest in seeing Tanzania continue to remain united and serve as a positive example.


The UN Secretary-General emphasized the importance of a meaningful and inclusive national dialogue aimed at addressing the root causes of the violent incidents that occurred on 29 October 2025, and at putting in place measures to prevent their recurrence.


He also reaffirmed the United Nations’ full support to Tanzania’s ongoing efforts, including support during and after the completion of the mandate of the Commission of Inquiry established in the United Republic of Tanzania.

GUTERRES: TANZANIA NI MFANO WA AMANI DUNIANI.

 

"Tanzania inaendelea kuwa mfano wa amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote."


Hayo ni maneno ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa AntΓ³nio Guterres, alipokuwa akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo.


Ujumbe huo uliwasilishwa na Mjumbe Maalum, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Katibu Mkuu Guterres alitambua kuwa sifa ya Tanzania kama nembo ya amani ilipimwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Hata hivyo, alipongeza uthabiti wa nchi katika kudumisha umoja na utulivu wa kitaifa.
Alisisitiza ni maslahi ya Umoja wa Mataifa kuiona Tanzania ikiendelea kubaki imara na kutumika kama mfano chanya.


Katibu Mkuu huyo wa UN pia alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa yenye maana na jumuishi. Lengo la mazungumzo hayo ni kushughulikia mizizi ya matukio ya vurugu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025, na kuweka mikakati ya kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo.


Alihitimisha kwa kuthibitisha msaada kamili wa Umoja wa Mataifa kwa jitihada zinazoendelea za Tanzania, ikiwemo kutoa msaada wakati na baada ya kukamilika kwa kazi ya Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa nchini humo.


Tuesday, December 9, 2025

MIAKA 64 YA UHURU, TBN YATOA WITO KUDUMISHA AMANI.

 


Leo Desemba 9, tunapoadhimisha miaka 64 tangu Taifa letu lipate Uhuru, Tanzania Bloggers Network (TBN) inawapongeza Watanzania wote kwa kufikia hatua hii muhimu katika historia ya Taifa letu. Hii ni siku ya kutafakari safari tuliyotoka, mahali tulipo, na mwelekeo tunaoujenga kwa pamoja.


Waasisi wetu walituwachia zawadi kubwa—Uhuru. Lakini walituonya kuwa Uhuru hauwezi kuwa kamili bila kujitegemea. Leo tunakumbusha maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyewahi kusisitiza:


"Uhuru hauwezi kukamilika pasipo kujitegemea. Hatuwezi kuitwa huru kama tunategemea wengine kutupatia mahitaji yetu ya kimsingi."

 

Tujenge Taifa Letu – Tusiibomoe Tanzania


Kama mtandao wa habari za kidijitali, TBN inasisitiza kuwa mafanikio yetu kama Taifa yametokana na utulivu, umoja na mshikamano. Ili kuendelea mbele, tunahitaji kudumisha amani na maridhiano—nguzo muhimu za maendeleo.


Rais mstaafu Benjamin William Mkapa alituasa kwa busara:


"Amani si kitu cha asili; tunahitaji kuilinda na kuitunza kila siku. Bila amani, hakuna maendeleo ya kweli."


Tukikubali kuongozwa na chuki, uchochezi na vurugu, juhudi za waasisi wetu za kupambana na ujinga, umaskini na maradhi zitapotea. Tusiitumie mitandao au uhuru wa maoni kuharibu Taifa letu; tuitumie kulijenga.

Kila Zama na Kiongozi Wake – Tuunge Mkono Mageuzi


Kila kizazi kina wajibu wake. Kama alivyoeleza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi:


"Kila utawala na zama zake. Kila kiongozi na mchango wake katika ujenzi wa Taifa hili."


Katika awamu ya sasa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania inaendelea na mwelekeo wa 4R: Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding. Huu ni mwaliko kwa Watanzania wote kushiriki katika kujenga Taifa lenye maridhiano, mageuzi chanya na uimara wa kiuchumi na kijamii.


Tuna nafasi ya kuzungumza—basi tuseme kwa njia inayojenga, si inayobomoa. Kuthamini Uhuru ni kufanya kazi kwa bidii, kulinda amani, na kuacha kutumiwa kuharibu misingi ya Taifa letu.

 

TBN Inawatakia Maadhimisho Mema ya Miaka 64 ya Uhuru!


Tanzania Kwanza — Kazi, Utu na Mshikamano. Tusonge Mbele!


Beda Msimbe

Mwenyekiti, Tanzania Bloggers Network (TBN)

Monday, December 8, 2025

KENYA YAWAKATAA WACHOCHEZI WA MAANDAMANO YA TANZANIA

 







Mkuu wa Wilaya ya Oloililai, Rift Valley nchini Kenya Mhe. Andrew Mwiti Mathew amesema serikali ya Kenya haiungi Mkono wachochezi wa vurugu, ghasia na maandamano nchini Tanzania, akiahidi kuzuia Wakenya kuchochea na kushiriki kwenye vurugu na maandamano haramu.


Mhe. Mwiti amebainisha hayo leo Disemba 08, 2025 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, wakati wa Kikao cha ujirani mwema kilichofanyika Wilayani Longido, ikihusisha Kamati za Ulinzi za Mkoa wa Rift Valley na Mkoa wa Arusha, kama sehemu ya kuimarisha usalama na biashara kwenye eneo la mpaka wa Namanga.


"Sisi tuwahakikishie kuwa tumejipanga vizuri kuzuia wachochezi na mtu yeyote ambaye anaweza kuwa na nia ya kuja kujiunga na wale watakaokuwa wanapanga kufanya maandamano ambayo tayari tumehakikishiwa kuwa ni haramu kwani hayajaruhusiwa kisheria." Amesisitiza Mhe. Mwiti.


Awali katika maelezo yake,  Mhe. Makalla ameihakikishia Kenya kuwa serikali ya Tanzania imejipanga kikamilifu kuhakikisha hakuna vurugu wala matukio ya uvunjifu wa amani yatakayojitokeza kesho Jumanne Disemba 09, 2025, akiwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila ya kuwa na wasiwasi wowote.


Mhe. Makalla kadhalika katika kikao hicho ameahidi kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuhakikisha mpaka wa Namanga unaendelea kuwa salama pamoja na kuheshimu mipaka iliyopo na kuimarisha ufanyaji wa biashara kupitia mpaka huo ili kuleta tija kwa wananchi wa nchi hizo mbili.


TANZANIA AND U.S. MOVE TO FINALISE MAJOR INVESTMENT AGREEMENTS

 



Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, today held talks with the Acting United States Ambassador to Tanzania, Andrew Lentz, at Chamwino State House to advance key areas of bilateral cooperation and reaffirm the shared commitment to a modern, mutually beneficial partnership.

Ambassador Lentz—accompanied by the Counselor for Political and Economic Affairs—underscored Washington’s determination to reset the relationship and deepen economic, political, and security collaboration with Tanzania.

“The United States is committed to a partnership based not on aid dependency but on shared prosperity,” Ambassador Lentz said.

The discussions centred on ongoing negotiations involving major U.S.-linked strategic investments. Both sides acknowledged that talks on two flagship projects—the LNG Project and Tembo Nickel Project—are now in their final stages, pending formal signing. A third investment, the Mahenge Graphite Project, remains under active technical review.

President Samia welcomed Washington’s renewed commitment and assured the delegation that Tanzania remains focused on completing the remaining procedural steps.

“As a non-aligned nation, Tanzania is open, ready, and committed to working with all partners who respect our sovereignty and share our vision for prosperity,” the President said.
“These strategic projects are of national importance, and we are determined to finalise them so they can unlock jobs, investment, and sustainable prosperity for our people.”

The President highlighted that more than 400 American companies currently operate in Tanzania—reflecting the country’s stability, openness to investment, and strong historical ties with the United States.

Beyond investments, the meeting touched on broader areas of cooperation, including political stability, regional security, economic reforms, private-sector growth, health-sector partnerships, and people-to-people exchanges.

Ambassador Lentz congratulated President Samia for her vision and long-term national planning through Vision 2050, noting the U.S. Government’s readiness to support its implementation and reinforce the President’s 4R philosophy of reconciliation, resilience, reforms, and rebuilding trust.

Both sides agreed that strengthened communication, consistent engagement, and timely action on pending agreements are key to unlocking the full potential of U.S.–Tanzania relations.

This meeting marks a pivotal moment in redefining and revitalising the U.S.–Tanzania relationship. The reaffirmed commitment from both governments signals the emergence of a modern, transparent, private-sector-driven partnership rooted in shared prosperity, mutual respect, and long-term strategic cooperation.

Flagship Projects

1. LNG Project — Estimated Value: USD 42 Billion
A transformative natural gas development involving leading international energy companies. The project aims to unlock Tanzania’s vast offshore gas reserves, boost national revenue, create thousands of jobs, and position the country as a major global LNG supplier.

2. Tembo Nickel Project — Value: USD 942 Million
A major critical-minerals investment in Ngara focused on nickel—an essential component in electric-vehicle batteries. The project will support global clean-energy supply chains, stimulate industrialisation, and expand Tanzania’s export base.

3. Mahenge Graphite Project — Value: USD 300 Million
One of the world’s largest high-grade graphite deposits, positioned to serve the fast-growing battery and renewable-energy sectors. The project will reinforce Tanzania’s role as a leading supplier of battery-grade minerals.

TANZANIA NA MAREKANI ZASONGA MBELE KUKAMILISHA MAKUBALIANO MAKUBWA YA UWEKEZAJI

 



Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Tarehe 08 Desemba 2025, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, katika Ikulu ya Chamwino, kujadili maeneo muhimu ya ushirikiano na kuimarisha dhamira ya pamoja ya kujenga ushirikiano wa kisasa na wenye manufaa kwa pande zote mbili.

Balozi Lentz—aliyefuatana na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa na Uchumi—amesisitiza dhamira ya Washington kuhuisha mahusiano na kuongeza kina cha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya mataifa haya mawili.

“Marekani imejitolea kujenga ushirikiano usiotegemea misaada, bali unaojengwa juu ya ustawi wa pamoja,” alisema Balozi Lentz.

Mazungumzo yamejikita katika hatua za majadiliano ya miradi mikubwa inayoongozwa na kampuni za Marekani.

Pande zote mbili zimekubaliana kuwa majadiliano ya miradi miwili ya kimkakati—Mradi wa LNG na Mradi wa Tembo Nickel—yamefikia hatua za mwisho kabla ya kutiwa saini rasmi. 

Uwekezaji wa tatu, Mradi wa Mahenge Graphite, unaendelea kufanyiwa uchambuzi wa kiufundi.

Rais Samia ameukaribisha upya msimamo wa Marekani na kuhakikishia ujumbe huo kuwa Tanzania itaendelea kusimamia hatua zote zilizobaki ili kukamilisha taratibu na kufungua njia ya utekelezaji wa miradi hiyo.

“Kama taifa lisilofungamana na upande wowote, Tanzania iko wazi, tayari na imejitoa kufanya kazi na washirika wote wanaoheshimu uhuru wetu na kushiriki katika dira yetu ya maendeleo,” alisema Rais Dkt. Samia.


“Miradi hii ni ya umuhimu mkubwa kwa taifa, na tumejidhatiti kuikamilisha ili iweze kufungua ajira, uwekezaji, na ustawi endelevu kwa wananchi wetu.”

Rais pia alibainisha kuwa zaidi ya kampuni 400 za Marekani kwa sasa zinafanya shughuli zao nchini Tanzania—kiashiria cha uthabiti wa nchi, mazingira mazuri ya uwekezaji na historia ya muda mrefu ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa haya mawili.

Mbali na uwekezaji, mazungumzo yamegusa maeneo mapana ya ushirikiano ikiwemo utulivu wa kisiasa, usalama wa kikanda, mageuzi ya kiuchumi, ukuaji wa sekta binafsi, ushirikiano katika afya na programu za kubadilishana uzoefu kati ya wananchi wa nchi hizi mbili.

Balozi Lentz amempongeza Rais Samia kwa maono na mipango madhubuti ya muda mrefu kupitia Vision 2050, na kusisitiza kuwa Serikali ya Marekani iko tayari kuunga mkono utekelezaji wake pamoja na kuimarisha falsafa ya 4R ya Rais—maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya imani katika utawala.

Pande zote zimekubaliana kuwa mawasiliano ya karibu, ushirikiano wa mara kwa mara, na hatua za haraka katika kukamilisha makubaliano yaliyosalia ni muhimu katika kufungua uwezo kamili wa uhusiano kati ya Tanzania na Marekani.

Kikao hiki kinawakilisha hatua muhimu katika kufafanua upya na kuhuisha mahusiano kati ya Tanzania na Marekani. Dhamira ya pamoja iliyothibitishwa na serikali zote mbili inaashiria mwanzo wa ushirikiano wa kisasa, wazi, unaoongozwa na sekta binafsi—ukijengwa juu ya ustawi wa pamoja, kuheshimiana na ushirikiano wa muda mrefu wa kimkakati.

Miradi Mikuu ya Kimkakati

1. Mradi wa LNG — Thamani Inayokadiriwa: Dola Bilioni 42

Mradi mkubwa wa kugundua na kuchakata gesi asilia unaohusisha kampuni kubwa za kimataifa za nishati. Mradi huu unalenga kufungua hazina kubwa ya gesi iliyopo baharini, kuongeza mapato ya taifa, kuunda maelfu ya ajira na kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kama mchezaji muhimu wa LNG.

2. Mradi wa Tembo Nickel — Thamani: Dola Milioni 942

Uwekezaji mkubwa wa madini muhimu eneo la Ngara unaolenga nikeli—kiungo muhimu katika utengenezaji wa betri za magari yanayotumia umeme. 


Mradi huu utaimarisha minyororo ya kimataifa ya nishati safi, kuchochea viwanda na kuongeza pato la mauzo ya nje.

3. Mradi wa Mahenge Graphite — Thamani: Dola Milioni 300

Chanzo kikubwa duniani cha madini ya graphite yenye ubora wa juu, yenye umuhimu katika uzalishaji wa betri na teknolojia za nishati jadidifu. Mradi huu utaimarisha nafasi ya Tanzania kama mtoa huduma mkuu wa malighafi muhimu za viwanda vya kisasa vya betri.

TPA YASAINI MAKUBALIANO KUANZA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO

 

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa (kushoto) na Rais wa Kampuni ya Africa Global Logistics ( AGL) Ltd Bw. Philippe Labonne ( kulia) wakisaini hati ya makubaliano ( MoU) ya ushirikiano wa Usanifu na Ujenzi wa gati tatu mpya katika Bandari Bagamoyo, tarehe 6 Disemba,2025 Makao Makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam.

Na Albert Kawogo


MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imesaini hati ya Makubaliano ( MoU) na Kampuni ya Africa Global Logistics ( AGL) Tanzania Ltd yenye Makao Makuu yake Nchini Ufaransa ambayo ni kampuni tanzu ya MSC, kwa ajili ya usanifu, Ujenzi na uendeshaji wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo. 


Hati hii ya makubaliano ( MoU) imesainiwa tarehe 6 Disemba,2025 Makao Makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa na Rais wa AGL Philippe Labonne.


Bw. Mbossa amesema, kusainiwa kwa hati ya Makubaliano ni ishara ya utayari wa kuanza kwa mradi wa Bandari mpya ya Bagamoyo ambapo kwa kuanzia AGL itaanza usanifu na Ujenzi wa gati tatu mpya za Kisasa kati ya 28 zinazotatajiwa kujengwa katika Bandari hiyo pamoja na gati mbili mpya za Kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam. 


“Tunategemea kuanza Ujenzi wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo mapema mwezi Januari na pia tunawakaribisha Wawekezaji wengine wa ndani na wa nje katika Mradi huo ambapo lengo ni kuleta mapinduzi makubwa katika Shughuli za Kibandari Nchini” Amesema Bw. Mbossa. 


Kwa upande wake Rais wa AGL Bw. Philippe Labonne anasema wameamua kuingia makubaliano na TPA na kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa nchi yenye Amani, Usalama na mazingira bora na tulivu ya uwekezaji iliyosehemu sahihi kijiografia kwa Sekta ya Uchukuzi na kuwa lango la Biashara Kitaifa na kimataifa. 


“ Ninaamini Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi kimaendeleo ikiwa na mtaji Mkubwa wa watu wakatimu na mtazamo Chanya na pia ni lango la kuingilia nchi nyingi barani Afrika na kuyafikia masoko ya kimataifa, Naamini ushirikiano huu utafungua mambo mengi ikiwemo kutengeneza Ajira ambazo ni muhimu sana kwa maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla” Amesema Bw. Labonne. 


Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa gati mpya tatu utajengwa kwa miezi 36 ( miaka mitatu) na Kampuni ya AGL imepata nafasi hii ya kushirikiana na TPA katika Ujenzi huo kutokana na uzoefu wao kama kampuni kubwa ya huduma za usafirishaji na logistiki, inayotoa huduma kamili za usafirishaji, usimamizi wa mizigo, usafirishaji wa kimataifa na huduma za forodha, ikihudumia sekta mbalimbali kama uchimbaji, mafuta, chakula, na misaada ya kibinadamu, ikiwa sehemu ya kundi la kimataifa la AGL (zamani BollorΓ© T&L) na sasa wakiwa chini ya MSC.


Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa (kushoto) na Rais wa Kampuni ya Africa Global Logistics ( AGL) Ltd Bw. Philippe Labonne ( kulia) wakisaini hati ya makubaliano ( MoU) ya ushirikiano wa Usanifu na Ujenzi wa gati tatu mpya katika Bandari Bagamoyo, tarehe 6 Disemba,2025 Makao Makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam.


Wednesday, December 3, 2025

BARA LA AFRIKA TUNAHITAJI WANAHABARI MAHIRI KUKUZA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU.

 





Na Veronica Mrema - Pretoria 


Uandishi wa habari za sayansi kwa umakini na umahiri ni nyenzo muhimu ili kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii, kusaidia kukuza maendeleo ya tafiti na vumbuzi mbalimbali.


Bara la Afrika bado lina uhitaji mkubwa wa waandishi wa habari ambao wamejikita na wapo na umahiri katika kuwasilisha masuala ya sayansi kwa lugha rahisi zinazoeleweka kwa jamii.


“Kazi yoyote ile tunayoifanya [katika] sayansi ina maana tu pale inapofahamika vizuri kwa watu na jamii nzima,”.


Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Afrika Kusini Profesa Blade Nzimande amesema hayo alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 13 wa Waandishi wa Habari za Sayansi Duniani.


Mkutano huo WCSJ2025 unafanyika Pretoria Afrika Kusini kuanzia Disemba 1-5, 2025 ukiwa na kauli mbiu isemayo 'Uandishi wa sayansi, unaojenga uelewa na uthabiti wa sayansi na haki za kijamii'.


“Nilipoombwa kuja kufungua mkutano huu nilikubali mara moja kwa sababu ya umuhimu wa nafasi ya waandishi wa habari za sayansi katika kukuza sayansi,” amesema.


Ameongeza “Kwa hiyo waandishi wa habari ni daraja muhimu sana [lakini] hatusemi daraja lisilo na ukosoaji, hapana  bali daraja muhimu la kuielimisha jamii kuhusu sayansi.


“Kama bara, tunahitaji waandishi wa habari za sayansi wengi kwa sababu bado tunalo jukumu la kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu barani Afrika.


“Na mawasiliano ni sehemu muhimu ya hilo. Kwa mfano, tunayo mkakati wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Afrika [STISA 2034].


“.., ambao unalenga kukuza sayansi, utafiti na maendeleo barani Afrika jambo muhimu sana. Kwa hiyo tunathamini kazi mnayofanya, na ni muhimu sana,” amesema.


Amesema waandishi wa habari wanapaswa kusaidia Bara la Afrika kupambana na dhana potofu na ubaguzi katika namna sayansi inavyowasilishwa.


“Lazima tuwahusishe pia makundi yaliyotengwa wanawake, watu waliodhulumiwa au waliokuwa na historia ya ukandamizaji ili nao wawe sehemu ya mawasiliano ya sayansi.


“Moja ya hatari kubwa inayoweza kuua umuhimu wa sayansi ni kuifanya kuwa mradi wa viongozi au watu wachache.


“Sayansi haipaswi kuwa mradi wa tabaka la juu; lazima iwe mradi unaoeleweka na watu wote. Tunawahimiza kuhakikisha mnazingatia hilo kama waandishi wa sayansi,” amesema.


Prof. Nzimande ameongeza “Waandishi wa habari mnapaswa kukabiliana na changamoto ya taarifa za uongo [fake news].


“Hili ni mojawapo ya mambo hatari sana katika mawasiliano leo, mitandao ya kijamii ina mazuri na mabaya.


“Ni mazuri kwa kuwa kila mtu anaweza kupata taarifa  siku hizi karibu kila mtu anasema,” amesema na kuongeza  


“Mimi ni mtengeneza maudhui.” Lakini pia mitandao ya kijamii inaweza kusambaza taarifa za uongo haraka sana, jambo ambalo ni hatari.


“Katika sayansi, tunapaswa kupambana na taarifa za uongo, si tu katika jamii kwa ujumla, bali katika sayansi haswa kwa sababu inaweza kusababisha madhara makubwa.


Amesisitiza “Je, mnakumbuka wakati wa COVID jinsi taarifa za uongo zilivyosambaa?


“Leo kuna watu katika nchi kubwa wanaodai kwamba chanjo husababisha autism  jambo la uongo kabisa.


“Lakini likirudiwa na watu wenye mamlaka, linakuwa hatari zaidi. Hii ina maana kwamba lazima muwe jasiri kama waandishi.


“Mnapaswa kuwa jasiri na msiogope kuuliza maswali makubwa na muhimu,” amesema.


Teknolojia ya Akili Unde [AI] katika sekta ya habari pia si suala la kuliacha nyuma, amesisitiza,


“Tunahitaji kuingiza teknolojia mpya kama akili bandia katika kazi yenu, ili kuimarisha weledi na uwazi katika taaluma yenu.


“Tunapaswa pia kushughulikia tofauti katika namna sayansi inavyoripotiwa. Bara letu bado linatengwa katika mambo mengi.


“Mnachukua jukumu la kuhakikisha masuala ya sayansi yanawafikia Waafrika si hivyo tu.


“Bali pia kuhakikisha ubunifu, uvumbuzi na miradi ya sayansi kutoka  Afrika inatambulika ndani na nje ya bara,” amesema Prof Nzimande.


Diplomasia ya sayansi pia waandishi wa habari wanalo jukumu la kusaidia kuikuza ndani ya Bara la Afrika.


“Sayansi haina mipaka, na kwa sababu hiyo ina uwezo mkubwa wa kujenga mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi na mabara.


“Kama Afrika Kusini, tunaamini sana katika sayansi huria kwamba sayansi inapaswa kufikika zaidi na iwe wazi.


“Lakini lazima niseme kwamba waandishi wa habari za sayansi ni sehemu muhimu sana mjue au msijue katika kazi tunazofanya katika sekta ya sayansi.


“Bila ninyi, hatuwezi kuwafikia wale tunaopaswa kuwafikia,” amesema Prof Nzimande.

Tuesday, December 2, 2025

KARNE YA AI: 'SADC BADO KUNA PENGO LA MAWASILIANO YA SAYANSI'

 


Na Veronica Mrema - Pretoria 


Ulimwengu wa sayansi na teknolojia unasonga kwa kasi ya ajabu. 


Mataifa makubwa duniani yanawekeza kwenye ubunifu, utafiti wa kisayansi, na teknolojia za kisasa.


Teknolojia kama akili unde, kilimo cha kisasa na tiba za kibunifu zaidi zinabadilisha maisha katika mataifa makubwa duniani.


Karne ya akili unde [AI], roketi zinavuka anga, kuna uvumbuzi na gunduzi nyingi katika teknolojia mpya kwa kasi ambayo dunia haijawahi kushuhudia.


Mataifa makubwa yanawekeza, yanashirikiana, na yanapasha habari za sayansi kwa umma wao kwa kasi.


Lakini upande mwingine wa dunia, ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika [SADC], bado kuna pengo kubwa katika mawasiliano ya sayansi. 


Watafiti wanagundua, Serikali zinafanya miradi, taasisi zinavumbua, lakini taarifa 'hazitembei' kwa kasi inayohitajika.


Bado haziwafikii vema wananchi wake, hazijengi uelewa na hazifanyi sayansi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.


Ndani ya SADC, bado kuna pengo kubwa kati ya maendeleo ya ki-sayansi na jinsi ambavyo taarifa hizo zinavyowafikia wananchi.


"Kwa sababu nchi nyingi za SADC bado hazina mkakati wa mawasiliano katika masuala ya sayansi,".


Yameelezwa hayo na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika, Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (DSTI), Afrika Kusini Mwampei Chaba.


Ni wakati alipokuwa akifungua mdahalo wa siku moja wa waandishi wa masuala ya sayansi kutoka nchi 18 wanachama wa SADC.


Amesema kutokana na pengo lililopo katika upashanaji habari kuhusu maendeleo ya sayansi katika nchi hizo, ndiyo maana DSTI iliona vema kuwaleta pamoja waandishi wa habari na kufanya mdahalo huo.


Ni katika mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari za masuala ya sayansi [WCSJ2025] unaofanyika Pretoria nchini Afrika Kusini.


Akifungua mjadala huo, aliweka wazi changamoto kubwa wanazokutana nazo waandishi wa sayansi katika ukanda huu.


“Nchi nyingi katika SADC bado hazina mkakati wa ushirikiano katika mawasiliano kuhusu sayansi. Hiyo ndiyo sababu upashanaji habari za sayansi unakumbwa na changamoto nyingi.”


Ameongeza "Ukosefu wa mkakati huo unawafanya waandishi wengi kukosa ushirikiano wanaohitaji kutoka kwa Serikali zao.


"Mnashindwa kuwa karibu na watafiti, mnakosa mazingira rafiki ya kupata habari, pamoja na fursa za ufadhili au mwaliko kwenye matukio muhimu yanayohusu sayansi na uvumbuzi.


Amesisitiza "Kwa hivyo, katika nchi yako na unataka kupata ushirikiano kutoka Serikali [kuandika kuhusu habari fulani inayohusu sayansi] au unataka watambue kazi yako.


"Unataka kufadhiliwa kwa baadhi ya kazi zako. Unataka kualikwa kwenye matukio [kwa wengi wenu], itakuwa ngumu kwa kuwa hawana mkakati wa ushirikiano kuhusu hilo," amesema.


"Mkirudi nchini mwenu kafuatilieni hili kwa undani, nendeni mkaulize wizara [zinazohusika na masuala ya] sayansi, wizara za mawasiliano [iwapo] wameandaa mkakati?.


Hii ni mara ya kwanza kwa Bara la Afrika kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari za sayansi, afya, mazingira na mambo mengine yanayohusiana na hayo.


Mdahalo huo kwa ajili ya waandishi wa habari kutoka SADC ulilenga kuwaleta pamoja kujadiliana namna gani watasukuma mbele masuala ya sayansi ndani ya nchi zao kwa upashanaji habari.


"Hii ni warsha ya mafunzo yenye umuhimu mkubwa kwetu. wazo hili lilikuja kwetu mwaka 2022 tulipoandaa Mkutano wa Sayansi Duniani (World Science Forum).


"..,, ambao ulikuwa wa kwanza kuandaliwa barani Afrika. Kwa hivyo, tulitengeneza historia mwaka 2022 kwa kuandaa mkutano wa Sayansi Duniani barani Afrika. 


"Kisha tukaamua kuwa kuleta fursa kama hii barani Afrika bila waandishi, waandishi wa sayansi kuwa kwenye chumba, kungekuwa kupoteza. 



Ameongeza "Tunawezaje kuwasilisha kile tunachofanya katika mkutano, kama idara, kama serikali barani Afrika, kama taasisi zinazofanya utafiti, ikiwa hatuna uandishi wa sayansi kwenye chumba?


"Pia tuligundua kuwa waandishi wa sayansi bado hawana uwezo wa kutosha kuhusiana na uandishi na kuandika makala za sayansi. 


"Hivyo basi, tuliona hitaji la kuunda ushirikiano. Na Stellenbosch alishirikiana nasi kwa kiwango kikubwa. 


Amesema walianza kupanga warsha ya mafunzo, yenye vipengele vingi, ambayo itasaidia kujenga uwezo wa waandishi wa habari katika kuwasilisha kazi tunazofanya kwa ufanisi zaidi. 


"UNESCO ilifadhili baadhi ya wajumbe mwaka 2022, na imeendelea kuwa mshirika wetu tangu wakati huo. 


"Sekretari ya SADC pia imekuwa mshirika wetu, na tunashukuru sana michango waliyotoa kwa waandishi wa SADC kuungana nasi. 


"Chama cha Waandishi wa Sayansi wa Afrika Kusini (SASJA) pia kimeungana nasi, na sisi pia tuko kwenye mshirika mkubwa katika mkutano mwingine wa kihistoria," amebainisha,


Amesema mkutano wa WCSJ2025 walioandaa mwaka huu unatengeneza historia mpya nyingine na walitaka kuwa sehemu ya historia hiyo.


Amesema Afrika Kusini waliunda mkakati wa mawasiliano na ushirikiano katika masuala ya sayansi tangu mwaka 2015 na kwamba walichelewa mno kuunda.


"Taasisi yetu ilianzishwa Juni 2004, hivyo karibu miaka 11 baadaye, tu wakati huo tu tulikuwa na mkakati wa ushirikiano wa sayansi unaotekelezwa kwa sasa, na mchakato wa ukaguzi upo.


Amebainisha "Mwaka huu SADC ilishiriki katika G20. Tulikuwa Rais wa G20 na GSTI ilipanga kile kinachoitwa Wiki ya Utafiti na Ubunifu [Research and Innovation Week]. 


"Pia tulipitisha hati maalumu inayoitwa Azimio la Ushirikiano wa Sayansi wa G20 (G20 Science Engagement Resolutions). 


"Hati hiyo inahimiza nchi za G20 kuweka sayansi kati-kati ya jamii inahimiza kuongeza ufahamu katika jamii zetu kuhusu thamani ya sayansi, na kuwasilisha sayansi kwa njia jamii zinaweza kuelewa.


"Kwa nini tunapaswa kufanya hivyo? Ni kwa nini hii ni muhimu? Sayansi haifadhiliwi vya kutosha, na hili ni changamoto katika jamii nzima.


Amesisitiza "Ikiwa thamani ya sayansi haifahamiki, ikiwa athari ya sayansi haijulikani kwa serikali zetu, jamii zetu, wafadhili wetu na wachangiaji.


"Basi mpango wa kufafanua ni ninyi walioko hapa. Ninyi ndio midomo yetu. Ninyi ndio mabalozi wetu wa kuwasilisha sayansi kwa jamii. 


"Mara sayansi itakapofahamika, mara thamani ya sayansi itakapothibitishwa kwenye hatua za vitendo, kwenye jamii, kwenye vijiji.


"Basi mna nafasi nzuri ya kupata ufadhili kutoka Serikalini, ufadhili kutoka kwa wafadhili na kadhalika. 


"Kwa hivyo, jukumu lenu ni muhimu sana, na tunategemea ninyi kusaidia kuunganisha pengo," amesema na kuongeza, 


"Napenda kuwahimiza kwamba katika wiki hii, mchukue fursa ya warsha nyingi zinazofanyika kuhamasisha sayansi. 


"Matumizi ya data, sita-sita kusema kwamba sayansi inapaswa kuwa kati-kati ya jamii, elimu, viwanda, ili kuendesha maendeleo kwa ujumla. 


"Na haiwezi kuwa katikati ikiwa ninyi hufahami jinsi ya kuwasilisha sayansi. Nami naamini hatuhitaji kuwa wanasayansi ili kuelewa sayansi. 


"Sayansi inapaswa kufafanuliwa kwa mtu wa miaka 85 na mtoto wa miaka 5. Bila kutumia maneno magumu. 


Amesisitiza "Ikiwa mtu hawezi kueleza, ikiwa mwanasayansi unayemhoji hawezi kueleza sayansi yao kwa njia unayoielewa, basi hawafanyi kazi nzuri. 


"Na pia unapaswa kuwa na uwezo wa kuhimiza wanasayansi kuzungumza na kuwasilisha sayansi kwa njia kila mtu anaweza kuelewa.


Amehoji "Je, unajua waandishi mashuhuri wa sayansi barani Afrika? Kwa nini haingewezekana iwe wewe?


"Kwa nini haingewezekana iwe wewe?” aliuliza, akiwahimiza washiriki kuwa wao wenyewe wanaweza kuwa waandishi mashuhuri wa sayansi Barani Afrika. 


“Kuna waandishi wa sayansi mashuhuri duniani kote, lakini sio barani Afrika. Afrika inahitaji sayansi kwa maendeleo zaidi kuliko kanda nyingine yoyote duniani. 


"Hivyo basi, tufanye lengo letu kuwa na waandishi mashuhuri wa sayansi katika jamii zetu, nchi zetu, ndani ya SADC na barani kote. 


Amesisitiza "Vinginevyo, mbona mko hapa? Kwa nini mko hapa ikiwa hatutumiwe kile tulicho nacho kuwasilisha sayansi na kuifanya iwe ‘fashionable’?”


Amehimiza waandishi wa habari kutumia vema majukwaa ya kidigitali kama fursa ya kufikisha taarifa muhimu zinazohusu sayansi kwa kundi la vijana ambalo kubwa lipo kwenye majukwaa hayo.


"Kila mtu yupo TikTok, kila mtu yupo YouTube, lakini lazima tuone maudhui ya sayansi pia kwenye TikTok au YouTube. 


"Tumia majukwaa haya maarufu kuwasilisha sayansi. Tuwafikie vijana walipo kwenye YouTube, Instagram na mitandao mingine na kuwapa elimu ya sayansi kwa njia wanayoielewa.”




Picha zote kwa hisani ya DSTI

Monday, December 1, 2025

TBN. YANG'ARA KIMATAIFA, VERONICA MREMA AINGIA JOPO LA MDAHALO MKUTANO MKUU WA DUNIA WA WAANDISHI WA SAYANSI.

 


PRETORIA, AFRIKA KUSINI


Kilele cha utambuzi wa uandishi wa habari za kidijitali nchini Tanzania kimethibitishwa baada ya Bi. Veronica Mrema, Mwanzilishi wa chombo cha habari cha M24 TANZANIA MEDIA na mwanachama mahiri wa Tanzania Bloggers Network (TBN), kuingia rasmi kwenye jopo la mdahalo katika Mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Waandishi wa Habari za Sayansi (WCSJ2025) unaofanyika jijini Pretoria. 


Hili si tu fahari kwa Mrema binafsi, bali ni heshima kubwa kwa TBN na tasnia nzima ya habari nchini, ikionesha kuwa kazi ya uandishi wa kidijitali inatambulika katika majukwaa makuu duniani.


Mrema yuko Afrika Kusini kuhudhuria mkutano huo mkuu unaotarajiwa kudumu hadi Desemba 5, 2025, baada ya kukabidhiwa udhamini maalum wa safari (Travel Grant) na Wizara ya Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu ya Afrika Kusini (DSTI). Udhamini huu ulikuja kama matunda ya utambuzi wa utendaji wake wa kipekee katika uandishi wa habari za kisayansi na afya, akibainishwa kuwa miongoni mwa wachache barani Afrika waliochaguliwa kwa heshima hiyo. Uwepo wake kwenye jopo la mdahalo unampa fursa adhimu ya kushiriki moja kwa moja katika kuunda mwelekeo wa mustakabali wa habari za sayansi duniani.


Akiwa anahutubia jukwaa la WCSJ2025 ambalo linakutanisha waandishi, watafiti, na wataalamu mashuhuri kutoka kote duniani, Veronica Mrema anatarajiwa kusisitiza kuwa tasnia ya habari za sayansi na afya barani Afrika inakua kwa kasi na kwa hivyo inahitaji sasa zaidi ya wakati mwingine uandishi wa weledi wa hali ya juu, ubunifu, na ushahidi wa ki-sayansi ili kufikisha ujumbe sahihi na wa kuaminika kwa jamii. 


Lengo lake kuu ni kuhakikisha uelewa sahihi wa sayansi unakuza maamuzi yanayoleta maendeleo, huku akitumia uzoefu wake kama kiongozi, ikiwemo nafasi yake kama Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DAR-PC) na Afisa Habari wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Selimundu Tanzania (SCDPCT), kutetea uandishi wenye tija.


Kutambulika huku kwa Mwanachama wa TBN kunaimarisha nafasi ya Tanzania katika uwanja wa uandishi wa habari za kisasa, kuashiria kwamba mchango wake katika upashanaji habari ni wa kiwango cha kimataifa.