Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo
cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, february 17, 2023.
................................................................
Na Athumani Shomari.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof
Adolf Mkenda, amesema serikali haitafumbia macho wale wote watakaojihusisha na
kuvujisha mitihani kwa namna yoyote ile.
Waziri Mkenda aliyasema hayo February 17, 2023
alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo
mjini Bagamoyo ambapo alisema kitendo
cha kuiba au kuvujisha mitihani ni kitendo cha dhulma dhidi ya wale wanaojituma
kufanya mitihani kwa akili zao.
Alisema tayari baadhi ya watu walioripotiwa
kujihusisha na wizi wa mitihani wameshaanza kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa
na jeshi la polisi na kuanza kuwahojiwa.
Prof. Mkenda amewapongeza polisi nchini kwa
kufuatilia matukio ya wizi wa mitihani na wahusika kuwachukulia hatua na
kuongeza kwa kusema kuwa, jeshi la polisi nchini linafanya kazi nzuri sana
katika kuhakikisha wizi mitihani unakomeshwa.
Aliongeza kwa kusema kuwa, walimu wanapaswa kuwa
na maadili mema ikiwa ni pamoja na kujizuia kabisa na vitendo vya udanganyifu,
wizi au kuvujisha mitihani kwa lengo la kujenga Taifa lenye watu wenye nidhamu,
na taaluma iliyopatikana kwa njia sahihi.
Waziri Mkenda ameutaka uongozi wa Chuo cha Wakala
wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kufundisha maadili pamoja malezi kwa
walimu wote watakaosomea uongozi wa elimu ili watakaporudi kwenye shule zao
wakasimamie maadili shuleni kwao kwa walimu walio chini yao pamoja na wanafunzi
wao.
Akizungumza mbele ya Waziri wa elimu, Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib alisema kasi ya uandikishaji wa wanafunzi wa
darasa la kwanza na ile wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shuleni
inaendelea vizuri katika wilaya hiyo na kwamba mpaka sasa wanafunzi wote
walioripoti ni asilimia 98.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia nafasi hiyo
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Huluhu Hassan
kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu hali iliyopelekea wanafunzi wote katika
wilaya hiyo kupata vyumba vya madarasa kwaajili ya kusoema.
Awali akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa majukumu
ya ADEM mbele ya waziri, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Masanja, amesema
ADEM ina majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kutoa mafunzo ya muda mrefu na
mfupi ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa viongozi na watendaji mbalimbali wa
elimu katika ngazi zote ikwemo Shule, Kata, Halmashauri, Mkoa, na Wizara.
Dkt. Masanja aliongeza kuwa, jukumu linguine ni
kufanya tafiti katika maeneo ya uongozi na usimamizi wa elimu ili kubaini na
kutafuta ufumbuzi wake lengo likiwa ni kutatua changamoto mbalimbali
zinazojitokeza katika sekta ya elimu.
Aidha, Dkt. Masanja alimueleza Waziri wa Elimu,
kuwa kozi za muda mrefu zinazotelewa chuoni hapo ni
1. Astashahada
ya Uongozi, Usimamizi na Utawala katika Elimu (Certificate in Education
Leadership, Management and Administration- CELMA) ambayo ni kozi mwaka mmoja na
ilianzishwa 2014.
2. Stashahada
ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (Diploma in Education Management and
Administration- DEMA) ambapo kozi hii ni ya miaka miwili, na ilianzishwa mwaka
2014.
3. Stashahada
ya Udhibiti Ubora wa Shule (Diploma in School Quality Assurance- DSQA) ambayo
hapo awali ilijulikana kama Stashahada ya Ukaguzi wa Shule (Diploma in School
Inspection-DSI) iliyoanzishwa mwaka 2014.
Alibainisha kuwa, katika kipindi cha miaka mitano
kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 jumla ya walimu 4,895 wamehitimu mafunzo ya Stashahada
za Uongozi, Usimamizi na Udhibiti Ubora wa Elimu.
Dkt. Masanja alisema pamoja na mafanikio
yaliyopatikana ADEM inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo.
1. Ufinyu
wa bajeti ya kuendeshea mafunzo ya muda mfupi na watendajina viongozi wa Elimu
wanaoteuliwa wakiwemo Maafisa Elimu, Maafisa Elimu Kata, Walimu wakuu, Wakuu wa
shule na Wadhibiti Ubora wa shule.
2. Baadhi
ya Walimu waliochaguliwa kujiunga na masomo yatolewayo na ADEM kukosa ruhusa ya
masomo kutoka kwa waajiri wao.
Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM,
ulianzishwa Tarehe 31 Agosti 2001kwa mujibu wa Sheria ya Bunge sura 245. Ambapo
kabla ya hapo Chuo hicho kiliitwa Taasisi ya MANTEP (Management Training for
Educational Personnel) ambayo ilianzishwa mwaka 1978 na katika kipindi hicho Taasisi
ya MANTEP ilijihusisha na utoaji wa Mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa Elimu ya
muda mfupi na muda mrefu kwa viongozi na watendaji wa sekta ya elimu.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akisalimiana na Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, katika viwanja vya ADEM.
Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala wa ADEM, Dkt. Emanuel Molel, (kulia) akimkaribisha Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipowasili katika viwanja vya ADEM.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akisalimiana Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipowasili katika viwanja vya ADEM.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akiangalia machaapisho yanayo onesha kazi za ADEM mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ADEM, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.
Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo cha ADEM Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akizungumza
katika Ukumbi wa Chuo hicho Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.
Viongozi wa Elimu Mkoa wa Pwani, Wilaya ya
Bagamoyo, Watumishi wa Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) na Kamati
ya Ulinzi na Usalama kwa pamoja wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea chuo
cha ADEM Bagamoyo jana Februry 17, 2023.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akimkabidhi Waziri wa Elimu, Taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya ADEM na machapisho mbalimbali yanayo onesha kazi za ADEM kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri- ADEM, Dkt. Naomi
Katunzi (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt za ADEM, Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kushoto)
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akijaribu zawadi ya T-shirt aliyopewa na uongozi wa ADEM, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, anaeshuhudia (katika) ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, (kushoto).