Monday, September 19, 2022

MUFTI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI YA BAKWATA MKOA WA SINGIDA

 No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (wa pili kushoto) akiongoza kuomba dua baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam  Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa katika hafla iliyofanyika Septemba 18, 2022. Kutoka kulia Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh Burhan Mlau, Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

..........................................

Dotto Mwaibale, na Philemon Mazalla-Singida

 

MUFTI wa  Tanzania sheikh, Dkt. Abubakar Zubeir, Septemba 18, 2022 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) Mkoa wa Singida


inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa.

Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi alisema amefurahishwa na kuridhishwa na hatua iliyochukuliwa ya kuanzisha ujenzi huo


kwani hayo ndiyo maendeleo yanayotakiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)

“Mimi na msafara wangu masheikh wote waliofika katika kutekeleza mambo yetu hapa Singida tumefurahishwa sana na jambo hili na haya ndio mambo yetu ya bakwata tunayoyazungumza sana kuhusu maendeleo” alisema Mufti Zuberi.

Mufti Zuberi alisema changamoto zote zilizotolewa katika hafla hiyo alisema baraza na viongozi wapo hivyo wanaona namna ya kuzishughulikia na kuwekana sawa kwani kila jambo lina taratibu zake namna ya kuzitatua.

Aidha Mufti Zuberi alisema jambo lililokubwa ni kwa waislam mkoani hapa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe kufanya mambo yao vizuri na kuondosha magomvi baina yao.

Taarifa ya ujenzi huo ikitolewa mbele ya Mufti ilieleza kuwa Mwezi Marchi 2022 Sheikh wa Mkoa wa Singida na Baraza la Masheikh waliunda kamati maalumu ili kuongeza nguvu ya ufuatiliaji wa eneo la ujenzi  na kufanikiwa kuipata ndani ya Masjid Taqwa


kwa idhini ya uongozi wa msikiti huo.

Ujenzi wa ofisi hiyo hivi sasa umefikia hatua ya linta kwa gharama ya Sh.8.2 Milioni, na kazi iliyobaki ni upauaji na umaliziaji ambapo fedha zilizokadiriwa kumalizia kazi hiyo ni Sh.14 Milioni.

Mufti akiwa njiani kwenda Singida mjini alisimama  wilayani Ikungi na kuomba dua kwenye eneo ambalo waislam wa wilaya hiyo wanatarajia kujenga Kituo


cha afya na baada ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi la ofisi ya Bakwata alikwenda kutembelea  Taasisi ya Majmaul Ahbaab iliyopo eneo la Unyakhindi Manispaaya Singida ambapo alipata fursa ya


kuzungumza na wanawake wa kiislam na kutunukiwa Tuzo ya heshima ya Kimataifa na Rais wa Taasisi hiyo Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akizungumza na Waislam wakati alipotembelea   Taasisi wa Majmaul Ahbaab.

No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akionesha Tuzo ya heshima baada ya kutunukiwa  na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh (kushoto).

No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (kushoto) akiwa na viongoziwengine katika hafla hiyo. Kutoka kulia ni  Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.